singidadodoma
JF-Expert Member
- Nov 11, 2013
- 4,394
- 1,536
Mara kwa mara nimekuwa nikiuliza huu umoja wa vyama vya upinzani wenyewe wameupa jina la Ukawa kama kweli viongozi wakuu wa umoja huu kama wapo sawa maana wanaonekekana kama vile wamelogwa na aliyewaroga amekufa au hajulikani alipo.
Hivi karibuni viongozi hao wa ukawa walikuta na kutoa malalamiko yao kwa umma juu ya rais Jakaya Kikwete kupuuza mapendekezo yao ya vyama vyenye uwakilishi bungeni (TCD).
Mapendekezo amabayo waliyataka rais ayabebe kama yalivyo ikiwemo kuvunja bunge la katiba lililokuwa likiendelea wakati huo ambapo rais aliwajibu kinaga ubaga kuwa atavunja bunge hilo kwa sheria ipi inayompa mamlaka ya kulivunja.
Pia ukawa walitaka ifanyike mabadilko ya sheria katika katiba hii tuliyo nayo ya mwaka 1977 ili kuvipa nafasi vipengele vitatu kabla ya uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwishoni mwa mwaka huu, vipengele vivyo ni pamoja na Tume huru ya uchaguzi, Mgombea Binafsi pamoja na kupinga matokeo ya urais.
Jambo ambalo wanashindwa kulielewa ukawa ni kuwa mambo yote hayo matatu yapo katika katiba pendekezwa ambayo wao wamekuwa vinara wa kuipinga katiba hiyo huku huko wakizunguuka nchi nzima katika majukwaa yao ya kisiasa.
Ukawa wamekuwa na mahesabu ya kutafuta maslahi ya kisiasa zaidi kwa silika ileile ya kulazimisha mambo bila ya kufiri kwa kina, nadhani hata rais analielewa hilo na ndio maana hajajielekeza katika makubaliano ya kulazimisha yasiyozingatia katiba wala sheria za nchi.
Narudia tena mambo yote hayo ambayo, Pro: Lipumba, Mbowe na Mbatia wanayoyataka yapo katika katiba pendekezwa, Japo ukawa walisusia mchakato huo na kutoka katika bunge hilo maalum la katiba, lakini wajumbe waliobaki kwa uchungu na uzalendo wa nchi yao waliyaingiza mambo hayo katika katiba pendekezwa.
Ajabu ukawa hao hao wanaotaka katiba pendekezwa ipigiwe kura ya hapana ili isipite halafu mnamshinikiza rais ayaingize yale mnayotaka yasipite mbona mnafanya mambo ya ajabu?
Ukawa mnapaswa kujua kuwa ikiwa katiba pendekezwa haitapita na nanyi pia madai yenu hayo matatu, ya Tume huru, Mgombea binafsi na kupinga matokeo ya urais hayatakuwepo kwakuwa tutaingia katika uchaguzi mkuu na sheria za sasa za uchaguzi za katiba ya mwaka 1977 zitaendelea kutumika.
Hamuoni kuwa mtakuwa mmewakosesha haki wananchi wanaotarajiwa kugombea kama wagombea binafsi? Kwa maslahi yaenu na vyama vyenu? Iwapi demokrasi mnayoihubiri hapo?
Hivi ukawa mnajua kuwa katiba pendekezwa ikipita ndio katiba iliyopitishwa itaanza kutumika na mambo hayo muhimu yatatungiwa sheria na bunge kwa mujibu wa masharti ya Mpito sura namaba 19 sehemu ya 6, kusudi katiba mpya ianze kutumika. Ambapo pia sheria mpya zitaanza kutumika kwa kipindi cha miaka mine baada ya kipindi cha mpito kukamilika na sheria zote husika kutungwa.