Narudia usichanganye siasa na afya kwa sababu utachemka.
Kwa maoni yako kipindupindu kimesababishwa na siasa mbaya za ccm?ina maana katika eneo kubwa la nchi ambalo halijapata kipindupindu basi kuna siasa safi za ccm?
Hiyo ndio conclusion uliyonayo...ndio maana nikakupa mifano ya magonjwa mengine yanayohusianishwa na Tabia na hali za kiuchumi na kukuonesha trends za magonjwa hayo.
Kama unachukulia sekta husika hazijafanya kazi kwa nini hujasikia kipindupindu Arusha au Mwanza au masaki mpaka sasa?
Ifike wakati tutenganishe siasa na utaalamu...hata USA na UK survellance ya kipindupindu inaendelea na haitashangaza kusikia kuna mlipuko wa kipindupindu.
Magufuli kaongelea afya kuhusu upatikanaji wa dawa...ni kweli dawa zinaibiwa especially katika level ya zahanati na vituo vya afya.
lakini kama ni mfuatiliaji Ilani ya CCM inaongelea kiuhalisia zaidi kuhusu universal coverage ya bima za afya,inaeleza kwa sasa tuko less than 20% na inaelekeza kuwa tunatakiwa kufika 30%,hizi ndio issues za Siasa ya Afya lakini ulivyokiongelea kipindupindu ulichanganya Afya na Siasa.