UKAWA Wapuuzwe!

UKAWA Wapuuzwe!

Paul Makonda

Member
Joined
Jul 8, 2011
Posts
97
Reaction score
186
Leo Nitatumia maneno makali kidogo ili tuelewane kiurahisi. Wapinzani wa Nchi hii ni "BAPHOON". Maana ya BAPHOON ni Watu au Kundi la Watu linalotumika Kwa Maslahi ya Mataifa Mengine Kuangamiza Taifa Lao. Wako Tayari Hata Kuchukua Mabomu na kulipua Nchi yao Wenyewe. Hawa ndio wanaojiita UKAWA (THE BAPHOON)

Imani namba Tano na namba nane za Chama Cha Mapinduzi kwa pamoja zinasema:
Cheo ni Dhamana, sitatumia cheo changu wala cha mtu mwingine kwa faida yangu na Nitasema Kweli Daima Fitna kwangu Mwiko.

Kwa tafsiri ya Imani ya Chama tunakubaliana na maneno ya Mwanahistoria wa zamani wa Uingereza Lord Acton aliyewahi kusema;

Power tends to Corrupt, and absolute power corrupts absolutely. Great men are almost always bad men

Yakimaanisha kuwa;

Madaraka yana tabia ya kuwaharibu walio nayo, na wenye madaraka makubwa Zaidi huharibika Zaidi kwa kuwa hata watu wema hugeuka kuwa wabaya wakishakuwa na madaraka

Na sisi Vijana Wazalendo tunasema;

Watu wenye Madaraka Makubwa Wakiharibiwa na hayo madaraka hulewa hayo madaraka na kuanza hata kutukana kudharau waliowapa madaraka hayo. Lakini wenye madaraka makubwa wanaojua kuwa madaraka yao ni dhamana, kwanza huwa wapore na wanyenyekevu na hubeba dhamana kubwa ambayo wao huona madaraka hayo ni Mzigo wala si zawadi.

Wapo wanaodhani kuwa Vyama vya Upinzani vipo kwa ajili ya Maslahi ya Taifa. Wapo wanaodhani Vyama vya Upinzani ndio mkombozi wao. Na wapo wanaodhani muarobaini wa matatizo ya taifa hili ya kiuchumi, kijamii na kisiasa ni vyama vya Upinzani. Ukweli halisi wamepotoka sana. Vyama vya Upinzani vipo kwa maslahi yao tu na vimekuwa ni dhaifu kiasi haviwezi kuaminiwa kupewa dhamana ya Uongozi wa Taifa hili.

Hatuna haja ya kuwaambia BAVICHA waombe radhi kwa matamshi yao yasiyo na adabu waliyoyatamka jana dhidi ya Rais wa Jamhuri na Waziri Mkuu kwa sababu tunajua wanadhani wako sahihi. Lakini tunajua wanajua hawako sahihi na wanafanya hivyo ili kuwaridhisha mabwana zao ambao wanawatumia wao kutengeneza mitaji yao kisiasa. Wao wanabaki tu kama kigenge fulani ambacho kama kikiachwa kikue na uwongo wake mwishowe kitaaminiwa na hapana shaka nchi hii ipo siku itaongozwa na Vichaa.

Tuelewe Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, ndiyo Lulu pekee iliyobaki Afrika ambayo imeundwa na sisi wenyewe , kwa hiari yetu wenyewe baada ya kukomboa sehemu zake mbili kutoka katika Ukoloni. Haiwezekani tuache Muungane uchezewe tu na wachache wetu ambao kinachowasukuma ni Uroho tu wa madaraka.

Tulipoanzisha Mfumo wa Vyama vingi, tulidhamiria kuwa na vyama vyenye nguvu za dhati ambazo ama zingekuwa kubwa kuliko CCM ili kuweza kuiwajibisha serikali sawasawa nayo iwajibike moja kwa moja kwa ujenzi wa taifa. Miaka 21 baada ya kuwa na mfumo wa vyama vingi, tumekuwa na vyama legelege ambavyo havina dira wala mwelekeo badala yake vimejikita katika uchochezi na ulaghai. Hali hii inatupa wasiwasi kama kweli hivi ni vyama vya siasa ama ni vikundi tu vya harakati vinavyofanya siasa. Watanzania wako tayari kuamini Upinzani lakini si kwa miaka hii ya karibuni,ni mpaka tutakapopata vyama vyenye nia thabiti ya kuleta maendeleo ya nchi hii huku vikithibitisha kwamba vitadumisha muungano wa nchi mbili serikali mbili na kuheshimu Katiba ya Nchi.

Chama Cha Mapinduzi kinabaki Imara na Msimamo thabiti wa Kuendelea na Jamhuri Muungano wa nchi mbili na Serikali Mbili. Azimio la kutaka serikali tatu si mara ya kwanza sasa. Azimio kama hili lilikuwepo Mwaka 1993 kwa hoja Binafsi ya Wabunge 55 (G55) iliyopelekwa na Mh. Njelu Kasaka Mbunge wa Chunya. Kwa kikao Cha Bunge cha August 24-27, Bunge liliridhia mchakato wa kuanzisha serikali ya Tanganyika. Lakini kwa Uthabiti wa CCM ambao ni imara sana sasa kuliko mwaka 1993, kilisimamia mfumo wa kubaki na Muungano wa Nchi mbili na Serikali Mbili. Msimamo wa CCM wa Mwaka 1993 ni thabiti sana sasa, hatuwezi kufufua Tanganyika isipokuwa tutatumia mfumo uliopo kutatua kero za Muungano zilizopo. Changamoto kubwa zinazotukabili ni za kiuchumi kuliko zilivyo za kijamii na muungano wetu sana una nia thabiti ya kijamii kuliko uchumi.

Demokrasia imechukua njia hadi sasa hata mifumo ya demokrasia imeanza kupuuzwa. Nasema inapuuzwa kwa sababu hata Vichaa sasa wanaweza kuamka tu na kutoa matamko yasiyo na kichwa wala Miguu. BAVICHA ni Vijana wadogo sana ambao hawawezi kuamka na kutoa matamko waliyoyatoa ila kwa kutumwa na Bwana zao. Na hao Bwana zao wanafadhiliwa na Mataifa ya nje ambay hayataki kuona siku moja AFrika inaungana na kuwa taifa moja kubwa. Namna pekee ya kufanikisha uovu huo mkubwa dhidi ya Afrika, ni kuibomoa Tanzania, na wenzetu hawa wapinzani wamekubali kutumika kama vibaraka wa kudidimiza Afrika.

Hatuoni Sababu ya Kukaa Kimya, Sitanyamaza kufumbia macho Ujinga huu. Nani kawatuma BAVICHA kutoa Matamko dhidi ya Rais na Waziri Mkuu? Nani kawadanganya kuwa eti Mchakato wanaoutaka UKAWA ndio Mchakato wanaoutaka Wananchi?

Unamsikiliza Mh. Lipumba, amejawa maneno kinywani mwake ya uchochezi tu wa kidini na ubaguzi wa wazi kabisa. Hizo zote ni hila ambazo kama zisipodhibitiwa kwa kuelezwa ukweli wake kama hivi, taifa litaangamia. Tumedhamiria kupambana na hili, hatutakaa kimya Mpaka watanzania watuelewe na wawapuuze wapinzani kwa lugha zao za uchochezi.

Kwa Nini wakatake kufanyia Mkutano Zanzibar kibanda Maiti na Si Dodoma maana wote walikuwepo hapa? Hivi wapi ni Karibu, Iramba kwa Tundu Lisu au Zanzibar (Unguja Kibanda Maiti)? kuna Umbali gani Hai kwa Mbowe au Tabora kwa Lipumba au Vunjo kwa Mbatia ukilinganisha na Zanzibar? Hawa waheshimiwa wasitake kulaghai Umma, kuna ajenda wameibeba ambayo hawataki kuisema. Warudi Bungeni waje wajenge hoja maana Katiba haitapatikana Majukwaani bali kwa kukamilisha Mchakato Bungeni na ndicho CCM tutakachofanya. Tunaendelea na Bunge na tunakamilisha Mchakato hata wasiporudi.

Ikiwa wao ni vyama vya kidemokrasia na nia yao ni kujenga demokrasia, kwa nini hawataki kukaa meza ya Mazungumzo? kwa nini wakimbie mkutano halali wa kidemokrasia wasikae hapo wajenge hoja hapo badala yake wanakimbilia eti kwenye mikutano ya hadhara? Hapo kuna walakini na demokrasia wanayohubiri. Anayehubiri demokrasia lazima awe wa kwanza kukaa meza ya mazungumzo. Mumewasikia wakitoa matamko kwamba hawako tayari kukaa meza ya mazungumzo na serikali wala CCM, hawa ni washari na wanatangaza shari na kisha wanatafuta huruma ya wananchi. Hiyo siyo demokrasia ni Vurugu. Uhuru bila mipaka i vurugu na Demokrasia bila Utaratibu nayo ni vurugu.

Tunazo tetesi kuwa hivi vyama vinafadhiliwa na wasiotaka kuiona Afrika ikiungana na kuwa jumuiya moja kubwa yenye nguvu. wanatafuta ucku na Mchana kuisambaratisha Afrika na namna pekee ye kuisambaratisha Afrika ni kuisambarataisha Tanzania kwa maana Tanzania ndiyo kinara wa Umoja wa Afrika. Kutumiwa kwao na Ukibaraka wao uendelee lakini tuko imara sana kulinda Muungano wetu. Hawa ni BAPHOON.

Lugha za kichochezi za wapinzani wananchi wamezisikia. Wamemsikia Prof. Ibrahim Lipumba akiweka matabaka ya watu kwa sababu za Kidini, wamemsikia Tundu Lisu akipandikiza chuki dhidi ya Mwalimu Nyerere na waasisi wa Muungano, Mumewasikia viongozi wa CUF, NCCR Mageuzi, wakifanya juhudi za kufitinisha watanzania kwa kauli zao ovu. Ufitini wa aina yoyote, uwe wa kidini, kikanda, kikabila au haiba ya watu hauna budi kupigwa vita kubwa na kila Mtanzania mpenda amani.

Wakumbuke, Chuki wanazozijenga sasa, itafika mahali zitakomaa na zikishakomaa zitaanza kuwa mwiba mkali kwao wao wenyewe. Kwa maana wakifanikiwa kupanda mbegu ya chuki miongoni mwa watanzania kwa namna yoyote ile, hakuna namna ambayo hao waliowapandikiza chuki watawapenda wao. Chuki yao itawala wao wenyewe na itaangamiza taifa. Hatuwezi kuacha hili litokee tukiangalia kwa macho yetu.

Taifa halitajengwa na watu waoga wala waongo na wafitini. Watanzania wenzangu tujikite katika kujenga uchumi na kujiletea maendeleo kwani tukiendelea kuwasikiliza "BAPHOON" hawa na kuacha shughuli zetu za kiuchumi, ni kujipotezea fursa tulizo nazo kwa faida ya wengine. Hawa wanawasumbua nyie mwasikilize, wao shughuli zao za NIGHT CLUBS, GUEST HOUSE ZAO, BAR ZAO, CASINO ZAO, DALADALA ZAO, MAHOTEL, na BIASHARA ZAO NYINGINE zinaendelea kuwaingizia Pesa na wanachofanya ni kuwajaza matumaini ya uwongo huku wao wanajaa MAPESA. Kwa kuwa wameamua kutumika na mataifa ya nje kuhujumu nchi yao, bado wanalipwa kwa kazi yao ya UFITINI. Mapato yao hayayumbi na wala hayatayumba.

Ewe Mtanzania Mwenzangu, Shtuka, Achana na BAPHOON.

Mungu Ibariki Tanzania
Paul C. Makonda
Katibu Uhamasishaji na Chipukizi UVCCM
Mjumbe Bunge Maalum la Katiba

0716696265


IMG_2546.JPG
IMG_2558.JPG
 
Unapenda kuiga sana we
Baada ya kusikia itarahamwe
Unakuja na lako
Hivi huna ubunifu? Acheni kukopi na kupaste

Vyama legelege halafu unachukua muda wote huo kuhangaika navyo? zitakuwa hazikutoshi wewe!
 
Kuvimbiwa kubaya sana; na hasa kuvimbiwa madaraka! Akina Jaji Warioba na Tume yake nao ni "BAPHOON"? Sidhani kama wewe ni "mkereketwa" au mzalendo kumzidi Jaji Warioba! Kumzidi Dr. Salim Ahmed Salim! Kumzidi Mzee Butiku! Kumzidi Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi na Jaji Mkuu Mstaafu Augustine Ramadhan! Sidhani kama una uzalendo kuzidi Tume zote zilizopita za akina Jaji Francis Nyalali, akina Jaji Kisanga, sidhani na haitakaa iwe hivyo.

Wewe u mtoto mdogo sana dogo, tena kinda kweli kweli. Tumia hekima acha kejeli hivi vyeo vinapita, vyama vinapita, taifa linadumu. Anyway, labda kwa sababu unaamini mtatawala milele sio ajabu ukaongea uliyoyaongea. Roma iliyoogofya mataifa ilikuja na kupita itakuwa kundi lenu! Babeli iliinuka, ikastawi, na ikasahaulika itakuwa kejeli zako. Kejeli hazijengi wala haziadabishi zaidi ya kubomoa. Ni ushauri wa bure; una hiari ya kuuchukua au kuachana nao ila wakati ndio utakaoamua.

===== UPDATES (Machi 02, 2017) =====

Uzi huu ulianzishwa Aprili 21, 2014 (miaka mitatu iliyopita) enzi hizo kabla aliyeuanzisha hajawa na madaraka makubwa aliyo nayo sasa. Tabia na mambo yaliyokuwa yamefichika sasa ni dhahiri. Kwa hakika muda ni mwalimu bora zaidi ...
 
Ujinga ni kitu kibaya sana, kwa utumbo ulioandika kwa hila za kizamani no wonder hao walio chini yako.
Asietaka Africa isiungane ni nani, na dhibitisha kama utaweza.
Tanganyika mmeimaliza, mmeiba kuanzia chumbani mpaka jikoni, mliposhindwa mmedalalia kwa thumuni, hamujali kitu, hamjali raia, wanafiki wa maneno na matendo
Mungu walaani hawa kunguni wenye hinda na choyo.
 
Amezoea vya kunyonga huyu, hana uwezo wa kuchinja kama wenzake tu, kimsingi tumewashtukia mna malengo ya kuitawala nchi kifalme, na kupitia marekebisho ya katiba mpya mtapotea kama mvuke, poleni sana. Watanganyika na wazanzibar now tunajua tunachokihitaji,


CCM na vibaraka wao hakika ndio wa kupuuzwa kwa kushindwa kuja na hoja za msingi juu ya hili. Tumechoka kushangilishwa kila mwaka katika kusherekea sikukuu ya uhuru wa Tanzania hali nchi hiyo haikuwa kupata uhuru popote, nina furaha kwa mara ya kwanza this december nitasherekea siku ya uhuru wa Tanganyika, my country.
 
Kwa Mara ya mwisho nchi hii kuongozwa na mtu mwenye akili timamu ilikuwa 8/December/ 1961 basi. Tangu 9/December/1961 ikachukuliwa na vichaa, magaidi, majangiri, mafisadi na wachumia tumbo wa ccm.

Ni miaka 54 sasa ccm imefika ukomo wa kufikiri tusitarajie jipya. CCM wanazani ubongo wao wakinyesi kila mtu anao. Ukichaa wa ccm musizani haujagundulika. Wananchi wamebaini nchi inaongozwa na vichwa boga.

Sasa badala ya kukataliwa na wananchi kwa unafiki wenu, munazani JWTZ ndo mbadala wa wapiga kura. hahahah........munachekesha sana.
 
Ninakuona kama kijana, uliyejaa maisha! What i would expect from you sio hoja na kioja kama ulivyoandika, Sisi wananchi tunafuatilia kila hatua mambo yanayotokea huko! Ni Mwanachama mwenzio mmoja tuu mpaka sasa ndie amechangia kama mtu anayejitambua na kuelewa uhitaji harisi wa kizazi chako wewe na watakaokufuata! The rest mkomko tuu, Ulisikiliza Maige aliongea nini? Tunategemea kama wewe unajiona msomi uwe introspective kiasi hicho! Dont ever think of your own interest when it comes kwa shughuli kama hiyo mliyokuwa mnaifanya ya kutunga katiba! openup your mind think globally, focus a thousand years to come!

Hapo ulichoandika depict how shortsited your focus lies on! Unajua wazungu wanatushindia wapi? They think a thousand years ahead, we are thinking two years ahead!! Hata hoja ya kuwa constitution ya miaka hamsini tuu ilikuwa hoja dhaifu, sasa angalia nyie wajumbe wenyewe na mawazo yenu!!

Kwa ushauli tuu, Tanzania ni muungano wa nchi mbili, Tanganyika and Zanzibar, sasa Wazanzibari wana wawakilishi, je nyie mnawawakilisha nani kama sio watanganyika? Hivi kwa mawazo yako unafikiri kwenye siasa kuna kuhurumia kama nyie mnavyofanya? It should stand as a win win kila uchao! So Wazanzibar they have a win, je sisi tuna nini? Kama sio loosers as per you and your group! Wakeup kijana it always has to stand a win win! For upande huu nao uwe una win sio loose every now and then!
 
Mtajitetea sana na vijembe vingi,lakini ukweli unabaki palepale kwenye rasimu ya Warioba wa Serikali Tatu,hayo ndio maoni ya Watanzania.Maoni ya CCM myaweke kwenye Katiba ya ccM,hii ya Watanzania imewashinda
 
Kuvimbiwa kubaya sana; na hasa kuvimbiwa madaraka! Akina Jaji Warioba na Tume yake nao ni "BAPHOON"? Sidhani kama wewe ni "mkereketwa" au mzalendo kumzidi Jaji Warioba! Kumzidi Dr. Salim Ahmed Salim! Kumzidi Mzee Butiku! Kumzidi Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi na Jaji Mkuu Mstaafu Augustine Ramadhan! Sidhani kama una uzalendo kuzidi Tume zote zilizopita za akina Jaji Francis Nyalali, akina Jaji Kisanga, sidhani na haitakaa iwe hivyo.

Wewe u mtoto mdogo sana dogo, tena kinda kweli kweli. Tumia hekima acha kejeli hivi vyeo vinapita, vyama vinapita, taifa linadumu. Anyway, labda kwa sababu unaamini mtatawala milele sio ajabu ukaongea uliyoyaongea. Roma iliyoogofya mataifa ilikuja na kupita itakuwa kundi lenu! Babeli iliinuka, ikastawi, na ikasahaulika itakuwa kejeli zako. Kejeli hazijengi wala haziadabishi zaidi ya kubomoa. Ni ushauri wa bure; una hiari ya kuuchukua au kuachana nao ila wakati ndio utakaoamua.

dudus,
Ushauri mwingine ni wa hekima mno haufai kuutoa tu kwa kila mtu. Kichaa ukimpa ushauri wa kuvaa nguo si unajisumbua? Umemwambia huyu kinda kuwa, ni kwa vile wanajiona watatawala milele? Huo ndio ukweli wenyewe. Alexander The Great hakuamini kuwa kuna siku Roma itaanguka.
Unategemea Lukuvi, Makonda na akina Mwingulu na Wassira waamini kuwa kuna siku ccm itakuwa chama pinzani?? Nawahurumia sana. Waache wazidi kujiamini
 
kijana acha dharau wewe fikiria warioba na wajumbe wa tume wameifanyia mambo mangapi nchi hii ukijilinganisha na wewe
 
Mhh nadhani anazo hoja za msingi ukisoma maelezo yake unayabaini tatizo lililopo hapa mnaanza matusi na kejeli kwa kuwa b flan kasema kwann tusimuulize maswali ya msingi kulingana na hoja yake akatufafanulia??
Ifike mahala iwe n mjadala mpana wa watu wenye mawazo tofauti ila yana mwelekeo wa kujenga na c kukosoa.
Wanasiasa mnaharibu sana hoja nyingi zenye maana kwa kuingiza malumbano yasiyo na maana kejeli na matusi.
Na hili ccm wamelitambua ndio maana wanakuwa na uelewa mpana wa kuchokonoa mada alafu wapinzani wanaporomosha kejeli na dhihaka mwisho wa siku n comedy.
Tufikie sasa mleta mada hata kama kaleta mada unayoiona ww haina mashiko mfanye aone hoja yake c ya msingi kwa kutaka aipambanue na akueleweshe c kejeli na dhihaka hatutafika hata siku moja tutabakia kulalamika majukwaani na kwenye mitandao kumbe cc wenyewe n tatizo kubwa.
 
Acha uhuni weye; fikiri kwanza,,,,,,,,,, baphoon ndiyo weye;;serikali tatu ndiyo inaelezeka vizuri;;;;; uko kama chemical Allly wakati wa vita vya iraq
 
ningekuwa mimi ndiye makonda ningeufuta huu uzi maramoja
 
Makonda atawasumbua sana kwenye siasa za taifa hili dogo anahoja sana.
 
Hivi haka ka-Pauli(ka-baphoon) baba yake nae alikuwa na wadhifa kwenye ukoo wa Panya au kamejipenyeza tu
 
Rais wa Tanzania hatatoka Kaskazini. Hiyo ni kauli kutoka UVCCM ilikuwa nzuri maana ilitoka ukanda wa kifalme.
Acheni kujilisha uongo.
 
Back
Top Bottom