UKAWA Wapuuzwe!

Inawezekana kuwa ukawa wana agenda yao ya siri sawa, lakini CCM nanyi agenda yenu kuendelea kutawala milele kitu ambacho kwa karne hii ni ndoto za mchana. Wananchi wakikukataeni hata msuke ghilba kiasi gani mtashindwa tu. Hakuna kioja cha mwaka mlichokifanya kama hiki cha kuunda tume yenu, kisha kuiapisha ifanye kazi. Tume kweli ikatekeleza hadidu rejea kama ilivyotumwa lakini cha kushangaza mnakana matokeo. Swali: JK alipoipokea rasimu tena alikuwa anatabasamu hii ilimaanisha unafiki au?. Nasema tena hata kama si ukawa akija yeyote anayeunga mkono maoni ya tume tutamuunga mkono kwa sababu anaheshimu wananchi ambao ndio msingi wa uongozi.

Paul Makonda wewe ni bwana mdogo sana kwa wazee kama Mhe, Judge mstaafu Joseph Warioba, Prof. Palamagamba, Prof Mwesiga Baregu, Hayati Dr. Sengondo Mvungi na wengineo.

Ona hata aibu ya kawaida tu. Kinachokufanya useme haya uliyosema hapa ni kuganga njaa tu hapo UVCCM wala hakuna hoja yeyote ya msingi kwenye waraka wote uliotunga hapa.

Watanzania tunaelewa siku hizi msitufanye wajinga. Kataeni maoni ya wananchi na sisi tunawakataa mchana kweupe.
 
Imani namba Tano na namba nane za Chama Cha Mapinduzi kwa pamoja zinasema:
Cheo ni Dhamana, sitatumia cheo changu wala cha mtu mwingine kwa faida yangu na Nitasema Kweli Daima Fitna kwangu Mwiko.

Makonda unapata wapi UJASIRI wa quote hiyo imani namba 5. Kweli umedhihirisha aliyezoea kuishi kwa UONGO hawezi kamwe kuishi kwa UKWELI.
 
Waanzilishi wa muundo wa serikali tatu ni wanzanzibar wenyewe-by Prof. Kabudi. Hitimisho la serikali tatu kuingizwa na kuja ni katiba ya Zanzibar ya 2010. Wanzanzibar woote ni Baphoon kwa maoni yako. Ukawa wameikuta hii movemewnt ilishaanza kitambo hata kabla ya Mh. Abudu Jumbe.

Ninyi CCM Dodoma, tunakumbuka kwamba, Wanzanzibar walipotambua kwamba CCM-Dodoma imewagawa wanzanzibar ili iweze kuwatawala milele; ndipo wakaja na maridhiano ya kitaifa (Taifa la Zanzibar), kwa siri Aman Karume na Maalim Seif wakaunda maridhiano hayo. Ninyi CCM-Dodoma mlipoona hilo mkajaribu kupinga na kuharibu mchakato wa maridhiano hayo. Wanzanzibar wakashika mwendo. Kisha ikaja katiba mpya ya wananchi wa Zanzibar 2010.

Maridhiano hayo yakaziba kila mpenyo wa CCM-Dodoma na watu wa bara kuingilia mambo na maamuzi ya wanzibar. Hao ndio kwa mujibu wa Makonda ni Baphoon.
 
Nyie mnajifanya waheshimiwa wote ni wadharauliwa...wananchi kibao tunawachora tunawaona wote mna tamaa na uchu tu na mkwanja wetu wa kodi,ushuru na tozo kama hizo ..Roho za mapinduzi tayari ziko mtaa,uhuru uko ndani yetu tunalala nao ghetto so ni swala la tym tu tumalize kazi pindi tuamshapo nyoyo zetu...
 
Endeleeni kuwaibia watanzania kwa kulipwa 300000 kwa siku kwa mipasho,kejeli, matusi na mbaya zaidi kwa uchakachuaji wa maoni ya wananchi juu ya katiba waitakayo! Interahamwe mnafahamika sana kwa udhalimu wenu!
 
Haka kajamaa kanahitaji angalau karudi shule maana kanaandika kanasarinasa(chekechea)
 
Hakuna ulichosema cha maana. Muungano wa tanganyika na zanzibar ulitengenezwa na Nyerere na karume,watanganyika wala wazanzibar hawakuulizwa kama wanautaka au hawautaki,hawakushirikishwa. Zama za kudanganyana zimeisha.

Tanganyika yangu ndio naitaka.
 
Duh maneno yangeweza kugeuka matendo Tanzania tungekuwa mbali sana kimaendeleo.
 
Huyu Makonda alijuaje kama Ukawa wanakenda kwenye guest houses kama hawakukutana huko? Nisaidieni. Huyu jamaa anataka aungwe mkono kwenye nini?
 
Ili tuongee kama watu wenye busara na sio kubwabwaja na kuonyesha ni nani mwenye vocabulary kubwa zaidi ya matusi, ni vema tukatumia data na evidence..,
  • Je unazo evidence kwamba wanatumia na mataifa ya nje ?
  • Je tuwapuuze sababu wanachoongelea / wanachotetea hakifai au tuwapuuza sababu ni watu wa kupuuzwa ?
  • Je ni sababu zipi pia za kupuuza Tume iliyoleta ushauri wao kutoka kwa wananchi ? au nao wanatumiwa kutoka nje ? na ni ma-baphoon (as you call them)
  • Je ni haki na busara kwa nyie kukiuka maagizo ya Tume iliyotumia mapesa mengi ?, Je tuwaite nyie ni kina nani either kwa kuchagua Tume ambayo kama mnadai haikufanya kazi (basi uchaguzi wenu ulikuwa mbovu) au kama ilifanya kazi kwanini mkiuke ushauri wao ?
 
Hakuna haja ya kurumbana sana inatosha, ili twende mbele basi,Zanzibar ambao wanaonekana kama wao ndiyo wafalume
tuwaachie nchi yao na Tanganyika tuchukue nchi yetu.Serikali TATU ni unafiki hakuna muungano hapo.Kwanini tupigane kwa sababu ya unafiki?Tunahitaji kusonga mbele Tanzania ni zaidi ya CCM,CHADEMA,CAFU na wafuasi wake.Siyo lazima tuendelee kuwa pamoja ila tuachane kwa usalama tu basi.
 
Mleta mada ni Masihi DAjjal anaona kwa jicho moja tu.
 

Nilikuwepo nitarudi naenda msalani.....................................
 
Atakuja na thread,tume ya Warioba ipuuzwe,ikimaananisha maoni ya watanzania yapuuzwe!
 
Kwanza unatakiwa ujitambue kuwa huna point, ukishajua hilo usiandike maneno mengi sana kwani unazidi kujichora.
Sasa kwa ufupi ni kuw sisi wala nyie wajumbe wa BMK hatutakiwi kujadili msimamo wa ccm, tunatakiwa tujadili Maoni ya wananchi wenzetu kama yalivyowekwa pamoja na tume ya Jaji Warioba. Hakuna koti kingine, huo msimamo wenu mkajadili kwenye Nec yenu si kwenye bunge letu, ndiyo maana UKAWA wameamua kuwaachia ukumbi wa bunge ili mkae kama chama na vibaraka semi muamue halafu sisi tutawasubiri huku nje

MUNGU IBARIKI TANGANYIKA, MUNGU IBARIKI TANZANIA
 
Makonda atawasumbua sana kwenye siasa za taifa hili dogo anahoja sana.
Makonda yupi ni tofauti na yule aliyesema hela laki tatu haitoshi?? Uzalendo umetoka wapi?? Sisi tunawajua watetezi wetu si hawa wanao kataa hata uwazi wala uwajibikaji na wanaokataa yote tuliyowaambia kina Warioba bali wakaleta yao.
 
Nimesoma kila kitu ila sikuona hoja yako ya msingi iliyokutuma kuondaka maneno mengi kiasi hiki. Vija wengi mlioko CCM ni njaa zenu tu wala siyo kwamba mmefurahishwa na utawala bora ambao CCM inautumia kuendesha nchi. Ila mkumbuke mwisho wa siku mtakuwa kama 'TOILET PAPER' maana mnatumika bila hata ya kujijua. CCM inawenyewe ila wewe haumo nina huo uhakika.

Kila siku wananchi wanalia huduma mbovu, wizi wa kutisha wa viongonzi mpaka kufikia kutorosha wanyama Hai wewe mpuuzi kabisa unakuja kuandika ujinga kama huu. Nimekuchukia sana kwa upeo wako mdogo wa kuchambua mambo
Acha kutumka fungua kichwa na ujielewe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…