Ukiambiwa uchague kimoja kati ya hizi project za Kilimo utachagua ipi? na why?

Project ya Kilimo cha matunda
Mfano apple unachomeka machipukizi na wewe unakazana kulima tu mazao mengine humo humo mfano mahindi baada ya miaka mitatu unamiliki eka ya apple
Hivi ma apple kwa hapa bongo yanalimwa wapi?
 
Kwani hawana magonjwa ?
mi ninavyoona ufugaji wa nguruwe ni kama mali akiba
ukianza na malisho yao+madawa(chanjo) unakuja kumuuza kwa bei
ambayo haijapishana sana na gharama ulizotumia katika ufugaji wake
 
14. Kilimo cha matunda ya muda mfupi!
Why?

1. Ni aina ya mradi unaonivutia sana

2. Inaweza kuwa ajira ya kudumu. Nikiwa na "plots" kadhaa nitakazokuwa nikilima kwa kupokezana, matunda yanaweza kupatikana majira yote ya mwaka na hivyo kutoa ajira ya kudumu kwa watu kadhaa. Hiyo itasaidia "kujitengenezea" wateja wa kudumu.
 
Nachagua ufugaji wa ng'ombe wa maziwa.
Kwa sababu sinunui chakula, wanakula majani/nyasi ninazolima na ninahifadhi kwa ajili ya kiangazi na ninatumia gharama ndogo.
Ukiwa mzoefu ni mradi rahisi wenye faida kubwa.
Mkuu, umenishawishi kuhusu ufugaji wa ng'ombe wa maziwa. Nafikiri unaizungumzia "silage". Inaweza ikagharimu kiasi gani kwa mwaka kuandaa chakula cha ng'ombe watano?
 
Chasha farm hapo umepigaje ? Twende layers upande wa pili kiti moto....sababu ....project zote zina soko uhakika mzunguko utakuwa mzuri sana....chakula almost sawa sawa.....ukiweza tengeneza cha kiti koto ...na ukiweza zaidi tafuta formula ya layers....anza kuku 1000...na kitimoto majike 10....utanielewa after 2yrs
 
Inategema na eneo ila kwa huku kusini katika utafiti wangu ,ningechagua namba 1&2 .

Huku hamna maziwa wala nyama yaani ni dili sana hivyo vitu. Kusini haswa Mtwara
Kwa mkoa wa mtwara misitu ni adimu mno utafugia wapi?
 
Ufugaji wa nguruwe unalipa sana, hasa ukipata mbegu nzuri. Maana nguruwe ukimtunza vizuri, akiwa na umri wa kuanzia miezi 8. Siyo chini ya 250,000. Hiyo inategemeana na maeneo uliyopo.
 
Nachagua ufugaji wa ng'ombe wa maziwa.
Kwa sababu sinunui chakula, wanakula majani/nyasi ninazolima na ninahifadhi kwa ajili ya kiangazi na ninatumia gharama ndogo.
Ukiwa mzoefu ni mradi rahisi wenye faida kubwa.
Mkuu, unatumia mbinu gani kuhifadhi? Una mitambo ya kuchakachia ili iweze kukaa muda mrefu bila kuharibika?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…