Nyamuma iliyobaki
Member
- Jun 25, 2023
- 10
- 24
Zanzibar iwe mkoa wa Tanzania au kuwe na serikali ya Tanganyika.Zote tunajua kuwa katiba yetu inamapungufu mengi. lakini sasa wewe kama mtanzania mzalendo ungepewa nafasi ya kuifanyia marekebisho ungetamani jambo gani jipya liwemo na lipi liondolewe ili Sisi kama Taifa tuwe na katiba nzuri kama nchi zingine.
Mimi nikipata nafasi hiyo nafuta tasisi ya kuzuia rushwa, kwa nini? Haiko fair, na inakamata walala hoi tu,mkubwa haguswi. karibuni kwa maoni!
Hii inatakiwa iwekwe kwenye hiyo miswaada ya sasa inayopelekwa bungeni.Kuharibu uchaguzi wowote au kuharibu kura kwa namna yoyote iwe ni kosa la uhaini... maana ni sawa na kupindua uongozi halali na kuweka viongozi mamluki.
Na pia kuwe na full transparency kwenye mchakato wote wa uchaguzi, kura ya mtu tuu ndio iwe siri.
Naunga mkono hojaTume huru ya uchaguzi na matokeo yote ya uchaguzi kupingwa mahakani.
IGP, TISS ,CAG ,CDF , CJ ziwe nafasi za kuombwa viwekwe vigezo watu kuomba hiyo kazi na wanao omba wafanyiwe usaili na kupigiwa kura na wabunge ili kuondoa mzigo kwa Rais na kufanya kazi kwa maelekezo vyombo viwe na uhuru wa kweli lakini vigezo na masharti vizingatiwe.
Zanzibar iwe ni mmoja ya mkoa wa Tanzania na kule kusiwe na Rais bali waziri mkuu wa pili au makamo wa pili wa Rais ndio ataongoza eneo la zanzibar atapigiwa kura pamoja na Rais na hatokuwa na mamlaka kumzidi Rais hivyo zanzibar itakuwa ni mkoa ndani ya Tanzania….
Hawakubali kwa sababu ni wezi wakubwa, wamepora mamlaka ya Dola na kugeuza sera za chama chao kuwa za taifa.CCM hawakubali lolote wao wanawaza wizi milele kwa Katiba hihi mbovu na kuwapa watoto na vijukuu vyao madaraka