D Metakelfin
JF-Expert Member
- Mar 23, 2017
- 3,399
- 3,666
Ndugu yangu wakati ukiwa unatekeleza mipango yako zipo changamoto zitakazokupitia na kukufanya hujihisi huna nguvu tena ya kuendelea. Kama wewe unaesoma ujumbe huu umekumbwa na jambo kama hili, nakusihi na kukupa nguvu kuwa unaweza ukanyanyuka tena na kuendelea na safari yako ya kuelekea kwenye mafanikio.
Hata magari pia yanaharibika yakiwa safarini kabla halijafika mahali yaendapo. Changamoto ni sehemu ya ushindi na ndo mana zimeletwa hili zitukomaze kabla ya kufika kileleni. Unapoweza kutatua changamoto zinazokutokea basi ni dalili nzuri ya kuyafikia mafanikio.
Leo nakwambia wewe ndugu yangu uliefeli shule kuwa unaweza kurudi shule na ukaendelea ulipoishia ili kufika kule ulikotaka kwenda, unaweza unaweza unaweza endapo tu utarekebisha makosa yako ya mwanzo ndugu yangu.
Naongea na wewe ulianzisha biashara na ukaishia njiani kwasababu duka liliungua moto, nyanyuka tena ndugu yangu iko sehemu Mungu kakuandilia ndugu yangu.
Naongea na wewe unaetaka kuendeleza kipaji chako ila haujapata nafasi ya kuonekana, usichoke kufanya unachofanya hata kwa udogo. Jambo la msingi ni kuboresha unachokifanya. Ninaimani na wewe na ipo siku watu watakuona.
Ninaimani na nyie, Mungu bado hajamalizana na nyie bado anakitu kikubwa kuja Kwenu.amkeni tena na mpambane na changamoto kwa kutafuta habari sahihi za changamoto inayokukumba. Ipo siku utafika unapotaka kufika.
Crédit:zingo
“Start where you are. Use what you have. Do what you can.”