Derrickmuyeya
New Member
- Sep 13, 2021
- 1
- 2
Kwa muda nafikiria,fumbuzi sijapatia,
Madhila yanotukia,lini mwisho kufikia,
Huru yakatuachia,mazuri kuyafurahia,
Huwa nawaza ni nani,kumfunga paka kengele.
Kwa siku zinavyosonga,ni mengi yanaibuka,
Tunashindwa kuyapinga,tunazidi kuteseka,
Akili zetu mefunga,na kuwaza tumechoka,
Huwa nawaza ni nani kumfunga paka kengele.
UVIKO janga dunia,Tanzania kaingia,
Madhara katuletea,nguvu kazi teketeza,
Kwa tabu utapumua,gonjwa likikuingia,
Huwa nawaza nani atamfunga paka kengele.
Gonjwa huyu katufika,Mengi yametutokea,
Mechachamaa hakika,madhara katuletea,
Wazungu wahangaika,kirusi kukiondoa,
Huwa nawaza nani kumfunga paka kengele.
Naamua kuandika,ujumbe kuufikisha,
Tuone yalotufika,kuondoa fanikisha,
Kuweza kubadilika,mazuri kushughulisha,
Huwa nawaza nani kumfunga paka kengele.
Chanjo zimepatikana,ili weze kutukinga,
Watu bado wazozana,kama ni kweli zakinga,
Mwafaka hujapatikana,watu bado wanapinga,
Huwa nawaza nani kumfunga pake kengele.
Maneno mengi yajaa,mzungu ni lake lengo,
Waafrika kutuondoa,wazibe na letu pengo,
Rasilimali kutumia,waweke yao majengo,
Huwa nawaza nani kumfunga paka kengele.
Yafaa kuwaambia,wenzangu watanzania,
Kujikinga inafaa,gonjwa hili kukimbia,
Chanjo hizi zatufaa,yatupasa kuzitumia,
Huwa nawaza nani kumfunga paka kengele.
Mwisho nataka usia,msumari shindilia,
Menibidi waambia,tusije tukajutia,
Chanjo ni zitatufaa,jitokeze kutumia,
Hakika ukichanja utamfunga paka kengele.
~Innocentfaraja6320
Kalamu ya kinda✍
Madhila yanotukia,lini mwisho kufikia,
Huru yakatuachia,mazuri kuyafurahia,
Huwa nawaza ni nani,kumfunga paka kengele.
Kwa siku zinavyosonga,ni mengi yanaibuka,
Tunashindwa kuyapinga,tunazidi kuteseka,
Akili zetu mefunga,na kuwaza tumechoka,
Huwa nawaza ni nani kumfunga paka kengele.
UVIKO janga dunia,Tanzania kaingia,
Madhara katuletea,nguvu kazi teketeza,
Kwa tabu utapumua,gonjwa likikuingia,
Huwa nawaza nani atamfunga paka kengele.
Gonjwa huyu katufika,Mengi yametutokea,
Mechachamaa hakika,madhara katuletea,
Wazungu wahangaika,kirusi kukiondoa,
Huwa nawaza nani kumfunga paka kengele.
Naamua kuandika,ujumbe kuufikisha,
Tuone yalotufika,kuondoa fanikisha,
Kuweza kubadilika,mazuri kushughulisha,
Huwa nawaza nani kumfunga paka kengele.
Chanjo zimepatikana,ili weze kutukinga,
Watu bado wazozana,kama ni kweli zakinga,
Mwafaka hujapatikana,watu bado wanapinga,
Huwa nawaza nani kumfunga pake kengele.
Maneno mengi yajaa,mzungu ni lake lengo,
Waafrika kutuondoa,wazibe na letu pengo,
Rasilimali kutumia,waweke yao majengo,
Huwa nawaza nani kumfunga paka kengele.
Yafaa kuwaambia,wenzangu watanzania,
Kujikinga inafaa,gonjwa hili kukimbia,
Chanjo hizi zatufaa,yatupasa kuzitumia,
Huwa nawaza nani kumfunga paka kengele.
Mwisho nataka usia,msumari shindilia,
Menibidi waambia,tusije tukajutia,
Chanjo ni zitatufaa,jitokeze kutumia,
Hakika ukichanja utamfunga paka kengele.
~Innocentfaraja6320
Kalamu ya kinda✍
Upvote
3