Ukicheka na nyani:polisi watatu wafa ajalini

Lole Gwakisa

JF-Expert Member
Joined
Nov 5, 2008
Posts
4,768
Reaction score
2,361
"Polisi watatu wafa katika ajali" Nipashe ya 20/12/2008[/B]Ajali hii ni ya kufunga mwaka wana JF,
Polisi watatu wameuwawa na dereva wa basi pale Kibaha , na dereva huyo kukimbia.
Dereva alisababisha ajali Kibaha na kuua.Akakimbia na basi pamoja na abiria wake mpaka Mikese kilometa karibu 100, mwanaume anakimbia tu!
Yamekuwapo malalamiko mengi kuwa Polisi wa Barabarani wamekuwa kama wanafanya mchezo wa kuigiza katika kudhibiti madereva wazembe, hasa katika barabara zetu za kwenda mikoani.
Hii ajali iliyotokea ya kusikitisha lazima iwaamshe wenzetu wa Polisi Usalama Barabarani kuwa kucheza cheza na hao madereva wa mabasi, hasa yaendayo Mbeya ndiko kuewamaliza wenzao watatu.
Ajali za mabasi ruti hii ya Mbeya zimekithiri, na dereva kuua Polisi na kuondoka, huo ni ujasiri wa pekee.
Polisi Usalama barabarani lazima wajiulize utendaji wao umekaa vipi ili kudhibiti matukio kama haya.
Leo limewatokea , tena wenyewe, ni suala la kusikitisha.
 
.....na sasa wanavuna mabua. Hii yote ni kwaajili ya kuendekeza kitu kidogo. Mpaka hapo watakapo acha kuchukua rushwa ndogondogo kupitia kwenye vifaili wanavyojifanya vya kuchorea ramani na kuandikia namba za magari, madereva makatili wataendelea kuwagonga mpaka watakapojirekebisha
 
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…