Ukidaiwa ukashindwa kulipa ukapelekwa Mahakamani unaposomewa mashtaka ya madai mdaiwa akikana maana yake nini?

Ukidaiwa ukashindwa kulipa ukapelekwa Mahakamani unaposomewa mashtaka ya madai mdaiwa akikana maana yake nini?

Mung Chris

JF-Expert Member
Joined
Sep 12, 2017
Posts
3,391
Reaction score
3,849
Wazoefu wa sheria njoni mnisaidie tafsiri, mfano mtu amekopa akabakisha rejesho 2 akaacha kulipa, mwisho wa siku walio mkopesha wakaamua kumpeleka mahakamani, alivyo somewa mashtaka tu akakana kuwa hadaiwi akaambiwa na hakimu asaini sehem ndani ya faili lake, aliye mkopesha akaambiwa awasilishe ushahidi ( Mkataba wa mkopo ambao upo, na mtu aliyemkabidhi mkopo huo) kesi ikaahirishwa hadi tarehe 16 ili kusikiliza ushahidi.

Sasa wakuu Hii inakaaje kwa wajuzi wa sheria huyu bwana amejiingiza kitanzini au baadae atakubali kuwa anadaiwa, je endapo ataikubali mikataba ya kudaiwa baada ya kuonyeshwa na huku ameshakana kwa mara ya kwanza kuwa hadaiwi hii kesi itakuwaje.
IFAHAMIKE KUWA JAMAA ANAKOPESHA KWA SABABU AMESAJILI BIASHARA HIYO NA ANALIPA KODI YA SERIKALI KAMA KAWAIDA.

Petro E. Mselewa Njoo bingwa
 
Wazoefu wa sheria njoni mnisaidie tafsiri, mfano mtu amekopa akabakisha rejesho 2 akaacha kulipa, mwisho wa siku walio mkopesha wakaamua kumpeleka mahakamani, alivyo somewa mashtaka tu akakana kuwa hadaiwi akaambiwa na hakimu asaini sehem ndani ya faili lake, aliye mkopesha akaambiwa awasilishe ushahidi ( Mkataba wa mkopo ambao upo, na mtu aliyemkabidhi mkopo huo) kesi ikaahirishwa hadi tarehe 16 ili kusikiliza ushahidi. sasa wakuu Hii inakaaje kwa wajuzi wa sheria huyu bwana amejiingiza kitanzini au baadae atakubali kuwa anadaiwa, je endapo ataikubali mikataba ya kudaiwa baada ya kuonyeshwa na huku ameshakana kwa mara ya kwanza kuwa hadaiwi hii kesi itakuwaje.
Dawa ya deni kulipa, na si wala kuleta janja janja na kisha baadae kukimbilia JF kuomba msaada.

LIPA DENI LA WATU
 
Dawa ya deni kulipa, na si wala kuleta janja janja na kisha baadae kukimbilia JF kuomba msaada.

LIPA DENI LA WATU
Chiwaso sidaiwi mimi elewa uzi sijadaiwa na sitaki kudaiwa, nilichokiona leo mahakamani na kushuhudia ndio nauliza nipate ufafanuzi kwa hilo
 
Katika kesi yoyote jukumu la kuthibitisha kuwa kuna claim ni la mlalamikaji;mimi sio mwanasheria ila kwa kesi za madai kwa kawaida unapoenda mahakamani unapaswa ujue kwanza uliweka dhamana gani?Mkataba ulikuwa unasemaje?Je ukishindwa kulipa nini kitatokea?So kukana au kukubali kunategemea hayo yote.Mfano kama umeweka kitu bond na mdai wako anacho unapokana kwamba hudaiwi ni uzwazwa kama unadai kwamba umemaliza deni utapaswa kuthibitisha hilo.Ila maswla ya mahakamani huwa yanategemea na wewe na anayekushtaki nani anawezamshikia hakimu chni vizuri
 
Mfano kama umeweka kitu bond na mdai wako anacho unapokana kwamba hudaiwi ni uzwazwa kama unadai kwamba umemaliza deni utapaswa kuthibitisha hilo
Ok nashukuru mfano hakuweka kitu bond alidhaminiwa tu na mumewe na mwenyekiti wa mtaa alisaini sehem yake kumtambulisha mtu huyo kuchukua mkopo inakuwaje ila ushahidi wa mkataba anao na finger print aliyoiweka. risiti za rejesho 2 kati ya 4 tu ndio anazo maana ndio alilipa, itakuwaje
 
Mkuu hiyo ni njia ya kukuchosha wewe mdai,kesi itakua ndefu huku mkimalizana kimya kimya

Apo lazima uwe na ushahidi wa kutosha kwamba unamdai
 
Ok nashukuru mfano hakuweka kitu bond alidhaminiwa tu na mumewe na mwenyekiti wa mtaa alisaini sehem yake kumtambulisha mtu huyo kuchukua mkopo inakuwaje ila ushahidi wa mkataba anao na finger print aliyoiweka. risiti za rejesho 2 kati ya 4 tu ndio anazo maana ndio alilipa, itakuwaje
Alipe tu aache kupoteza muda na kujichosha na mwishoe aje kujikuta analipa na gharama za kesi.Mume wake ndo atamlipia na kwa kawaida kwa sababu ni mtu binafsi basi mali zake binafsi zitapigwa mnada na kuuzwa
 
mi pia sio mtaalamu wa sheria ila kesi za madai zina utata sana, ata kama kuna mkataba ukiweka wazi kua huwezi kulipa kwa wakati huo na kama uliweka bond kitu ambacho kita adhiri jamii yako, kuna makubaliano nadhani yanaweza fanyika ya jinsi mdaiwa anaweza malizia deni lake
 
Pengine kuna technicality kaiona na anataka kuiexploit mfano upatu au kukopeshana uraiani hakutambuliki kisheria sasa huyu mtu akala hela kutoka kwenye upatu au kwa mtu aliyemkopesha.

Akifika mahakamani anaweza akakana, hata kama ukionyesha mkataba hiyo ni kwakua sheria inasema kua anayetakiwa kukopesha ni taasisi ya fedha na hata mhifadhi fedha ni benki hivyo hata huo mkataba ni batili kutokana na kua umevunja sheria.
 
Safi sana Castr kweli mikopo inatolewa popote pale mteja alipo ila Biashara hiyo imesajiliwa na inalipa kodi TRA kama kawaida sasa hana uhakika kama kweli imesajiliwa maana hajaona usajili je yeye kutoona ndio anweza akafikiria kuwa afanye hivyo maana ana uhakika kuwa haijasajiliwa atamlia iyo hela? tusaidie hapa
 
Mkuu unapanga kumzulumu mtu, I suggest you never do that aisee, "karma is a bitch"
 
Safi sana Castr kweli mikopo inatolewa popote pale mteja alipo ila Biashara hiyo imesajiliwa na inalipa kodi TRA kama kawaida sasa hana uhakika kama kweli imesajiliwa maana hajaona usajili je yeye kutoona ndio anweza akafikiria kuwa afanye hivyo maana ana uhakika kuwa haijasajiliwa atamlia iyo hela? tusaidie hapa
Inawezekana akawa anajua kua haijasajiliwa kwasababu taasisi rasmi hua ina taratibu zake za kufuatwa kwahiyo kama technicality anayotaka kuiexploit ni hiyo itakua ameona kua aliyemkopesha hatambuliki kisheria.

Ila technicality siyo hiyo tu.

Mfano taasisi ni rasmi ila jina la muomba mkopo lilikosewa au tarehe ilikosewa ingawa inaweza isimpe faida anayoikusudia ila anaweza kuing'ang'ania.
 
Yan mtu umetia fingerprint kisha hutaki kulipa deni, acha kumsumbua jamaa aliekupa hela, wakat una shida ulimuona yeye ndio msaada kwako, all in all ushahid huo utakutuia hatian na utalipa zaidi
 
ila ogopa mahakama za mtaani, hakuna kitu kibaya kama dhulma
 
Mdaiwa huwa hafungwi iwapo atakiri deni na kuhaidi kulipa taratibu. Ila ukikana kudaiwa na anaekudai akaonyesha ushahidi wa wewe kudaiwa kweli Mahakama ikithibitisha - Itagundua umefanya kosa la kusema uongo. Hakimu anaweza kutoa hukumu na ukitoka Jela lazima ulipe Deni la watu.
 
Back
Top Bottom