Ukienda kwenye guest au lodge yoyote usilale bila kuomba

Pdidy

JF-Expert Member
Joined
Nov 22, 2007
Posts
57,951
Reaction score
32,619
Haijalishi uko kikazi ama unaenda kusalimia familia, ndugu ,jamaa au marafikii.Nakujuza tu ukienda Lodge guest zozote kabla ya kulala sali.

Ndugu zile Lodge zina mambo mengi sana na kabla ujalala kuna mtu alitoka hapo,na pengine mfanya usafi angekwambia akiyokutana nayoo hata chumbani usingelala.

Humohumo yanafanyika uzinzi na uchafu kama wote.



Asubuhi njema
 
Sio huko tuu ata kwenye majumba yetu yakiwa mogofu watu waliyafanyia vituko ,pia nyumbani unaacha house girl na house boys wanaweza kukunjana popote na hayo maroho yakakuingia
 
Kama we ni Mtakatifu sana Bora uende na hema lala ukitaka lala.hotel, guest,loji zote ni chafu kiroho
 
Hakuna kitanda chochote cha hotel au loji ambacho hakijafanyiwa uzinzi so unaweza ukaondoka na maroho ya uzinzi ukawa mzinifu kuliko kwa tabia usiyo nayo awali
 
Unawez ukaend guest na mtoto wa watu,kuna michezo hutak hata kumfany Ila unakuta unamfany kumbe shida siy nyinyi ni mapepo yalioachwa na walioingia kabla yenu🤨🤨🤨
 
Nakubaliana na wewe kabisa.

Niliwahi kwenda Katavi kikazi na ilibidi kulala lodge.

Nilipoingia chumbani tu kwenye hiyo lodge nilihisi kama kusisimkwa na mwili ambapo kiuhalisia sikuweza kuelewa ni kwa nini lakini pia nafsi yangu ilikataa kabisa kulala mule ndani. Nilimuita muhudumu nikamwambia anibadilishie chumba. Kuuliza sababu nikamwambia sijakipenda tu kile chumba. Nikapewa chumba kingine.

Baada ya siku mbili nilipokuwa naondoka niikuwa napiga stori na yule muhudumu wakati nasubiria usafiri. Yule dada akaniambia kaka inaelekea una imani kubwa sana na Mungu wako, nikamuuliza sababu ya kusema hivyo; Jibu lake ndio lilinichosha kabisa. Akasema mwenye lodge huwa kila baada ya muda anakuja kufanya matambiko hapo lodge kwake na kile chumba nilichokikataa ndio huwa anakitumia zaidi.

Yule dada aliniambia kuwa ilishatokea mara mbili kwa wateja kukutwa wamefariki kwenye chumba hicho bila ya sababu za msingi na wakiwa peke yao.
Na sharti kubwa la mwenye lodge ni kuwa hicho kiwe ndio chumba cha kwanza kupewa mteja akija hata kama vingine vipo vitupu.

Binadamu huwa tunajisahau sana ila kuna mambo Mungu anatuepusha nayo bila hata ya sisi wenyewe kujua. Pengine ningeishia kuwa kafara kama ningelala humo.
 
Chura Kiziwi Juzi tu hapo si ulikua Katavi? Emu acha kutupanga
 
CHAI.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…