Blood of Jesus
JF-Expert Member
- Sep 19, 2016
- 4,486
- 8,098
Dawa ni kumwamini Yesu na kumpa maisha. Shetani alishashindwa na YESU wa msalaba. Kazi ya Calvari ni kazi kamilifu. uzao wa mwanamke (Yesu Kristo) ushamsaga nyoka (shetani) kichwa. MWANZO 3:15Nakubaliana na wewe kabisa.
Niliwahi kwenda Katavi kikazi na ilibidi kulala lodge.
Nilipoingia chumbani tu kwenye hiyo lodge nilihisi kama kusisimkwa na mwili ambapo kiuhalisia sikuweza kuelewa ni kwa nini lakini pia nafsi yangu ilikataa kabisa kulala mule ndani. Nilimuita muhudumu nikamwambia anibadilishie chumba. Kuuliza sababu nikamwambia sijakipenda tu kile chumba. Nikapewa chumba kingine.
Baada ya siku mbili nilipokuwa naondoka niikuwa napiga stori na yule muhudumu wakati nasubiria usafiri. Yule dada akaniambia kaka inaelekea una imani kubwa sana na Mungu wako, nikamuuliza sababu ya kusema hivyo; Jibu lake ndio lilinichosha kabisa. Akasema mwenye lodge huwa kila baada ya muda anakuja kufanya matambiko hapo lodge kwake na kile chumba nilichokikataa ndio huwa anakitumia zaidi.
Yule dada aliniambia kuwa ilishatokea mara mbili kwa wateja kukutwa wamefariki kwenye chumba hicho bila ya sababu za msingi na wakiwa peke yao.
Na sharti kubwa la mwenye lodge ni kuwa hicho kiwe ndio chumba cha kwanza kupewa mteja akija hata kama vingine vipo vitupu.
Binadamu huwa tunajisahau sana ila kuna mambo Mungu anatuepusha nayo bila hata ya sisi wenyewe kujua. Pengine ningeishia kuwa kafara kama ningelala humo.
JESUS IS LORD&SAVIOR