SoC02 Ukifa, utanikuta motoni nakusubiri

Stories of Change - 2022 Competition

Tanki

JF-Expert Member
Joined
Apr 7, 2013
Posts
538
Reaction score
246
" KILA NAFSI ITAUONJA UMAUTI, ndivyo yasemavyo maandiko.Lakini, moja kati ya habari ambazo hazinaga utamu kwenye ngoma za masikio ya wanadamu ni habari kuhusiana na KUFA / KIFO

Lakini, hebu jiulize maswali haya.
"Utakufaje?, wapi?, saa ngapi?, Itakuwaje hiyo siku na ni lini?, Na je, atakuwepo nani pembeni yako?. Atakuwepo Mtumishi Seperatus Kabwebwe au sheikh Hashim Rungwe?. Au utakuwa na bwana Willy Njau mwenye sifa ya kuwa daktari bingwa. Au atakuwepo Mzee Kufakunoga mganga maarufu kutoka Tanga?. Jiulize Familia yako itabaki na nani?, Nani atawajali watoto wako?, Ina maana yule mke wako mzuri kuliko wote duniani ndo atakuja kuolewa na kidume kingine?.

Hayo ni maswali tu, na yanaweza yasiwe na maana kabisa kwako, ila pengine kwa mwingine yanaweza kuwa na maana japo kidogo tu.

Na hivi, ni wangapi wataguswa na msiba wako?. Mimi binafsi kwa dhati kabisa nasema, ikitokea leo nimekufa, ninaamini watakaolia au kuhuzunika ni wachache sana.Wengi watafurahi.Ni kama vile naiona siku hiyo. Siku hiyo upepo utaongeza kasi ya kuvuma kwake. Kelele za oni za magari zitasikika kutoka kila kona ya jiji.
Madereva na makondakta watahisi kuipata ahueni yao, maana kisiki kitakuwa kimeng'oka. Kisiki cha mpingo mimi. Kisiki chenye SALE NYEUPE zilizokolea pasi na KOFIA kichwani.

Mpendwa, mimi ndiye mtu ninayeweza kumwambia mke wangu apike ugari, hata kama hela ya mboga sina, ila nikienda barabarani ndani ya dakika kumi tu ntarudi nyumbani na nyama kilo tatu, vitunguu, mafuta, nyanya, karoti n.k

Mpendwa, nikikusimamisha nitakutafutia kosa lolote lile kwenye gari yako na hauwezi kuchomoka.Uzuri ni kwamba watu wa siku hizi hamtaki mambo mengi. Mnajifanya hamtaki kupoteza muda. Na hapo ndo MTAJI wangu ulipo.Naweza nikakusimamisha na kukuelekeza pa kuweka gari arafu nisikufuate.
Mwishowe eti utaona nakuchelewesha na ndipo utakapoamua kunifuata wewe mwenyewe na kunishikisha noti ya shilingi elfu tano ndipo nakuruhu uende huku nikijifanya kukusema kinafiki. Tazama, nalikamata basi la kwenda mkoani kwa kosa la mwendo kasi. Dereva ananikamatisha elfu tano namuachia aondoe ndinga.
Anaendelea na mwendo kasi, mara paah! ajali mbaya inatokea. Watu wanaaga dunia. Nikilala huwa nahisi zile roho zikinililia ila sijali chochote.

Tazama, nipo barabarani naongoza magari.Bosi mmoja ananipigia simu kwamba anataka kuwahi nyumbani, hivyo anataka nimvute. Unajua namvutaje?. Namvuta hivi, yeye ananiambia tu anatokea upande upi. Kwahiyo cha kufanya mimi nitasimamisha magari ya upande mwingine na kuyaita magari ya upande anaokuja nao yeye. Wakati mwingine naita magari ya upande husika hadi yanaisha, barabara inakuwa tupu, ila kwa kuwa mlengwa bado hajapita nitaendelea tu kuita magari ya upande huo hadi bosi kubwa apite. Baada ya hapo lazima ujumbe wa muamala utaingia kwenye simu yangu.

Kuna rafiki yangu yeye huvaaga zile SALE za MABAKA MABAKA. Yeye amenipa jina la MZEE WA KUKAMUA. Na ni kweli daladala nazikamua sana sana sana. Tena makondakta siku hizi sisi wakamuaji wametupa jina la TAKUKURU. Utasikia dereva anamwambia kondakta......"Oya usifungue mlango mbele kuna TAKUKURU''.

CHOCHOTE KITU:
Hiki ndicho kitu kinachofanya niipende kazi yangu na sijawahi kujutia kuifanya kazi hii, maana ninachoamini UTAMU WA KAZI NI PESA. Huu ni mwaka wa ishirini na saba nipo barabarani na sijawahi kukamatwa nikipokea chchote kitu.

Wapendwa, mwambieni MAMA kwamba, hakuna akili kubwa inayotumika kwenye kumkamua mwananchi wake mlala hoi. Mwambieni mbona hakuna usiri mkubwa sana kwenye kupokea kwangu. Mbona wakati mwingine nashikishwa ka elfu tano kangu huku abiria wakiona. Ila uzuri ni kwamba abiria na hata wapita njia wanaweza wakaona, ila taasisi yake ya kupambana na hili jambo haioni.

Tazama, nakunywa sana pombe. Nafanya sana zinaa na hasa na wake wa watu.Najua nilivyo mchafu.Nilishalazimisha wanawake watoe mimba zangu ambazo hadi Leo ni zaidi ya kumi.
Miaka miwili iliyopita niliwahi kuua mtu.
Hivyo najua nikifa leo nitaenda wapi. Roho yangu hainiambii kwamba eti nami ni wa peponi. Ni wazi moto na adhabu kali vinaningoja.

Mpendwa, kama na wewe una matendo kama yangu basi naamini ukifa utanikuta motoni nakusubiri.
Nasema utanikuta kwasababu naamini mimi nitatangulia na wewe utanifuata.

Mpendwa, ulishiriki kwenye kum bambikizia kesi mlala hoi asiye na hatia na akafungwa.

Ulidhurumu mali ya mnyonge kisa tu wewe una misuli ya nguvu ya fedha.

Ndugu wakili msomi. Unasimama mahakamani kumtetea mtu ambaye ni kweli ametenda kosa na pengine ameshakuambia ukweli kwamba ametenda. Ila wewe unamtetea kwa mbinu zako ili tu ionekane hajatenda kosa.

Mwenye nyumba,gari, shamba, kazi nzuri, unawasimanga wasio navyo na kuwaona takataka.

Tapeli wa mitandaoni. Mwizi. Unatangaza unauza bidhaa, baada ya kutumiwa fedha unam bloki aliyekutumia na bidhaa haumtumii.

Unakumbuka uliwahi kumnyima kazi mtu mwenye vigezo vyote hapo ofisini kwenu na badala yake ukamleta ndugu yako ambaye hakuwa kabisa na vigezo?.

Ulipewa pesa, ili ukatoe ushahidi wa uongo mahakamani.

Ulipewa pesa ili ukatoe ushuhuda wa uongo kanisani.

Daktari, muuguzi msaidizi, hauwajali wagonjwa masikini.Mgonjwa analetwa akiwa na hali mbaya sana, ila wewe upo tayari kama kufa afe tu kisa hana pesa ya kukuhonga ili apatiwe matibabu.

Wakunga hospitalini wenye matusi au maneno ya hovyo kuwaambia wajawazito.

Mpo wengi sana, sana, sana. Nyinyi hapo juu ni baadhi tu. Ila ZINGATIENI KWAMBA WENYE TABIA KAMA ZANGU AU KAMA ZENU HAPO JUU, NAWAAMBIA, HAKIKA MTANIKUTA MOTONI. Pengine naweza kuwa mwenyeji wenu mwema sana. Huko tutalia na kusaga meno.

NINI TUFANYE?.
Uzima ndio unaofanya nayaandika haya. Wewe unayasoma maandishi haya kwasababu na wewe una uzima. Kwahiyo sisi sote bado tupo hai. KWANINI WEWE UJE MOTONI NA UNIKUTE MIMI?. Hivi hatuwezi kubadilika ili tu tusikutane huko motoni?. Bado tunao muda. Tutubu dhambi zetu na tuanze maisha mapya.

JAMII HAIWEZI KUENDELEA KAMA KILA MTU KWA NAFASI YAKE ASIPOTIMIZA WAJIBU WAKE.

Mungu anibariki mimi na wewe ili tusikutane kweli huko kunakoitwa MOTONI.
 
Upvote 22
nikweli ila nasikitika kwamba hata kama unauhai bado ulivyovitaja si sababu ya kukwepa moto uhai unao ila mbinu huna NAISHIA HAPA.
Mkuu, usiishie hapo. Nilitamani kama ungeendelea. OK, naomba niende kwenye hoja yako ya msingi. Kwanza nashukuru kwa kukili kwamba nilichokiandika kina ukweli.

SINA MBINU?: Mkuu, kwa mujibu wa nilichokiandika hapo juu na hasa nikiwa kama muhusika mkuu, ninayajua madhambi yangu. Uchafu wangu naujua vema. Umri huu nilio nao nimeona mengi na nimefanya mengi. Mkuu, watu kama mimi kwenye jamii tupo wengi. Wala rushwa, wezi, wazinzi, wauaji, wenye chuki, fitina, n.k
Mkuu, hayo yote jamii hayaipendezi jamii na hayampendezi MUNGU. Tunapotaka kubadilika ni lazima kwanza tukili makosa yetu. Ni lazima tuseme na mioyo yetu na nafsi zetu. Ni lazima TUTUBU kwamba tulikosea. Tutubu toba iliyo ya kweli. Baada ya hapo tuanze upya. Tuwe waadirifu. Tutekeleze wajibu wetu. Tuwe na hofu ya MUNGU. Mkuu, ukiwa mwadirifu hautaweza kumtetea muuaji ambaye tayari ameshakuambia ukweli kwamba aliua. Kusimama mahakamani kama wakili na kumtetea kwamba ajaua ni uadirifu?. Je, kufanya hivyo kuna mpendeza MUNGU na jamii?.
 
" KILA NAFSI ITAUONJA UMAUTI, ndivyo yasemavyo maandiko.Lakini, moja kati ya habari ambazo hazinaga utamu kwenye ngoma za masikio ya wanadamu ni habari kuhusiana na KUFA / KIFO

Lakini, hebu jiulize maswali haya.
"Utakufaje?, wapi?, saa ngapi?, Itakuwaje hiyo siku na ni lini?, Na je, atakuwepo nani pembeni yako?. Atakuwepo Mtumishi Seperatus Kabwebwe au sheikh Hashim Rungwe?. Au utakuwa na bwana Willy Njau mwenye sifa ya kuwa daktari bingwa. Au atakuwepo Mzee Kufakunoga mganga maarufu kutoka Tanga?. Jiulize Familia yako itabaki na nani?, Nani atawajali watoto wako?, Ina maana yule mke wako mzuri kuliko wote duniani ndo atakuja kuolewa na kidume kingine?.

Hayo ni maswali tu, na yanaweza yasiwe maana kabisa kwako, ila pengine kwa mwingine yanaweza kuwa na maana japo kidogo tu.

Na hivi, ni wangapi wataguswa na msiba wako?. Mimi binafsi kwa dhati kabisa nasema, ikitokea leo nimekufa, ninaamini watakaolia au kuhuzunika ni wachache sana.Wengi watafurahi.Ni kama vile naiona siku hiyo. Siku hiyo upepo utaongeza kasi ya kuvuma kwake. Kelele za oni za magari zitasikika kutoka kila kona ya jiji.

Madereva na makondakta watahisi kuipata ahueni yao, maana kisiki kitakuwa kimeng'oka. Kisiki cha mpingo mimi. Kisiki chenye SALE NYEUPE zilizokolea pasi na KOFIA kichwani.

Mpendwa, mimi ndiye mtu ninayeweza kumwambia mke wangu apike ugari, hata kama hela ya mboga sina, ila nikienda barabarani ndani ya dakika kumi tu ntarudi nyumbani na nyama kilo tatu, vitunguu, mafuta, nyanya, karoti n.k

Mpendwa, nikikusimamisha nitakutafutia kosa lolote lile kwenye gari yako na hauwezi kuchomoka.Uzuri ni kwamba watu wa siku hizi hamtaki mambo mengi. Mnajifanya hamtaki kupoteza muda. Na hapo ndo MTAJI wangu ulipo.Naweza nikakusimamisha na kukuelekeza pa kuweka gari arafu nisikufuate.

Mwishowe eti utaona nakuchelewesha na ndipo utakapoamua kunifuata wewe mwenyewe na kunishikisha noti ya shilingi elfu tano ndipo nakuruhu uende huku nikijifanya kukusema kinafiki. Tazama, nalikamata basi la kwenda mkoani kwa kosa la mwendo kasi. Dereva ananikamatisha elfu tano namuachia aondoe ndinga.

Anaendelea na mwendo kasi, mara paah! ajali mbaya inatokea. Watu wanaaga dunia. Nikilala huwa nahisi zile roho zikinililia ila sijali chochote.

Tazama, nipo barabarani naongoza magari.Bosi mmoja ananipigia simu kwamba anataka kuwahi nyumbani, hivyo anataka nimvute. Unajua namvutaje?. Namvuta hivi, yeye ananiambia tu anatokea upande upi. Kwahiyo cha kufanya mimi nitasimamisha magari ya upande mwingine na kuyaita magari ya upande anaokuja nao yeye. Wakati mwingine naita magari ya upande husika hadi yanaisha, barabara inakuwa tupu, ila kwa kuwa mlengwa bado hajapita nitaendelea tu kuita magari ya upande huo hadi bosi kubwa apite. Baada ya hapo lazima ujumbe wa muamala utaingia kwenye simu yangu.

Kuna rafiki yangu yeye huvaaga zile SALE za MABAKA MABAKA. Yeye amenipa jina la MZEE WA KUKAMUA. Na ni kweli daladala nazikamua sana sana sana. Tena makondakta siku hizi sisi wakamuaji wametupa jina la TAKUKURU. Utasikia dereva anamwambia kondakta......"Oya usifungue mlango mbele kuna TAKUKURU''.

CHOCHOTE KITU:
Hiki ndicho kitu kinachofanya niipende kazi yangu na sijawahi kujutia kuifanya kazi hii, maana ninachoamini UTAMU WA KAZI NI PESA. Huu ni mwaka wa ishirini na saba nipo barabarani na sijawahi kukamatwa nikipokea chchote kitu.

Wapendwa, mwambieni MAMA kwamba, hakuna akili kubwa inayotumika kwenye kumkamua mwananchi wake mlala hoi. Mwambieni mbona hakuna usiri mkubwa sana kwenye kupokea kwangu. Mbona wakati mwingine nashikishwa ka elfu tano kangu huku abiria wakiona. Ila uzuri ni kwamba abiria na hata wapita njia wanaweza , ila taasisi yake ya kupambana na hili jambo haioni.

Tazama, nakunywa sana pombe. Nafanya sana zinaa na hasa na wake wa watu.Najua nilivyo mchafu.Nilishalazimisha wanawake watoe mimba zangu ambazo hadi Leo ni zaidi ya kumi.
Miaka miwili iliyopita niliwahi kuua mtu.
Hivyo najua nikifa leo nitaenda wapi. Roho yangu hainiambii kwamba eti nami ni wa peponi. Ni wazi moto na adhabu kali vinaningoja.

Mpendwa, kama na wewe una matendo kama yangu basi naamini ukifa utanikuta motoni nakusubiri.
Nasema utanikuta kwasababu naamini mimi nitatangulia na wewe utanifuata.

Mpendwa, ulishiriki kwenye kum bambikizia kesi mlala hoi asiye na hatia na akafungwa.

Ulidhurumu mali ya mnyonge kisa tu wewe una misuli ya nguvu ya fedha.

Ndugu wakili msomi. Unasimama mahakamani kumtetea mtu ambaye ni kweli ametenda kosa na pengine ameshakuambia ukweli kwamba ametenda. Ila wewe unamtetea kwa mbinu zako ili tu ionekane hajatenda kosa.

Mwenye nyumba,gari, shamba, kazi nzuri, unawasimanga wasio navyo na kuwaona takataka.

Tapeli wa mitandaoni. Mwizi. Unatangaza unauza bidhaa, baada ya kutumiwa fedha unam bloki aliyekutumia na bidhaa haumtumii.

Unakumbuka uliwahi kumnyima kazi mtu mwenye vigezo vyote hapo ofisini kwenu na badala yake ukamleta ndugu yako ambaye hakuwa kabisa na vigezo?.

Ulipewa pesa, ili ukatoe ushahidi wa uongo mahakamani.

Ulipewa pesa ili ukatoe ushuhuda wa uongo kanisani.

Daktari, muuguzi msaidizi, hauwajali wagonjwa masikini.Mgonjwa analetwa akiwa na hali mbaya sana, ila wewe upo tayari kama kufa afe tu kisa hana pesa ya kukuhonga ili apatiwe matibabu.

Wakunga hospitalini wenye matusi au maneno ya hovyo kuwaambia wajawazito.

Mpo wengi sana, sana, sana. Nyinyi hapo juu ni baadhi tu. Ila ZINGATIENI KWAMBA WENYE TABIA KAMA ZANGU AU KAMA ZENU HAPO JUU, NAWAAMBIA, HAKIKA MTANIKUTA MOTONI. Pengine naweza kuwa mwenyeji wenu mwema sana. Huko tutalia na kusaga meno.

NINI TUFANYE?.
Uzima ndio unaofanya nayaandika haya. Wewe unayasoma maandishi haya kwasababu na wewe una uzima. Kwahiyo sisi sote bado tupo hai. KWANINI WEWE UJE MOTONI NA UNIKUTE MIMI?. Hivi hatuwezi kubadilika ili tu tusikutane huko motoni?. Bado tunao muda. Tutubu dhambi zetu na tuanze maisha mapya.

JAMII HAIWEZI KUENDELEA KAMA KILA MTU KWA NAFASI YAKE ASIPOTIMIZA WAJIBU WAKE.

Mungu anibariki mimi na wewe ili tusikutane kweli huko kunakoitwa MOTONI.
Hongera jmn karibu pia kusoma
 
Hongera jmn karibu pia kusoma
Shukrani mkuu
 
Mkuu, usiishie hapo. Nilitamani kama ungeendelea. OK, naomba niende kwenye hoja yako ya msingi. Kwanza nashukuru kwa kukili kwamba nilichokiandika kina ukweli.

SINA MBINU?: Mkuu, kwa mujibu wa nilichokiandika hapo juu na hasa nikiwa kama muhusika mkuu, ninayajua madhambi yangu. Uchafu wangu naujua vema. Umri huu nilio nao nimeona mengi na nimefanya mengi. Mkuu, watu kama mimi kwenye jamii tupo wengi. Wala rushwa, wezi, wazinzi, wauaji, wenye chuki, fitina, n.k
Mkuu, hayo yote jamii hayaipendezi jamii na hayampendezi MUNGU. Tunapotaka kubadilika ni lazima kwanza tukili makosa yetu. Ni lazima tuseme na mioyo yetu na nafsi zetu. Ni lazima TUTUBU kwamba tulikosea. Tutubu toba iliyo ya kweli. Baada ya hapo tuanze upya. Tuwe waadirifu. Tutekeleze wajibu wetu. Tuwe na hofu ya MUNGU. Mkuu, ukiwa mwadirifu hautaweza kumtetea muuaji ambaye tayari ameshakuambia ukweli kwamba aliua. Kusimama mahakamani kama wakili na kumtetea kwamba ajaua ni uadirifu. Je, kufanya hivyo kuna mpendeza MUNGU na jamii?.
ni sawa ila ulinielewa kwa upande wako, haswa nilichomaanisha pia kinaweza kikawa nje ya hoja zako ni vizuri tusimamie hapo
 
Sawa mkuu, ila ingekuwa vema kama ungeweka bayana ulichokimaanisha ambacho pengine kinaweza kikawa nje ya hoja zangu kama ulivyosema. Nia ni kuijenga jamii
 
Makala nzuri sana. Neema ya Mungu ingalipo, Tutubu. Mkuu tunga kitabu.
 
" KILA NAFSI ITAUONJA UMAUTI, ndivyo yasemavyo maandiko.Lakini, moja kati ya habari ambazo hazinaga utamu kwenye ngoma za masikio ya wanadamu ni habari kuhusiana na KUFA / KIFO

Lakini, hebu jiulize maswali haya.
"Utakufaje?, wapi?, saa ngapi?, Itakuwaje hiyo siku na ni lini?, Na je, atakuwepo nani pembeni yako?. Atakuwepo Mtumishi Seperatus Kabwebwe au sheikh Hashim Rungwe?. Au utakuwa na bwana Willy Njau mwenye sifa ya kuwa daktari bingwa. Au atakuwepo Mzee Kufakunoga mganga maarufu kutoka Tanga?. Jiulize Familia yako itabaki na nani?, Nani atawajali watoto wako?, Ina maana yule mke wako mzuri kuliko wote duniani ndo atakuja kuolewa na kidume kingine?.

Hayo ni maswali tu, na yanaweza yasiwe maana kabisa kwako, ila pengine kwa mwingine yanaweza kuwa na maana japo kidogo tu.

Na hivi, ni wangapi wataguswa na msiba wako?. Mimi binafsi kwa dhati kabisa nasema, ikitokea leo nimekufa, ninaamini watakaolia au kuhuzunika ni wachache sana.Wengi watafurahi.Ni kama vile naiona siku hiyo. Siku hiyo upepo utaongeza kasi ya kuvuma kwake. Kelele za oni za magari zitasikika kutoka kila kona ya jiji.

Madereva na makondakta watahisi kuipata ahueni yao, maana kisiki kitakuwa kimeng'oka. Kisiki cha mpingo mimi. Kisiki chenye SALE NYEUPE zilizokolea pasi na KOFIA kichwani.

Mpendwa, mimi ndiye mtu ninayeweza kumwambia mke wangu apike ugari, hata kama hela ya mboga sina, ila nikienda barabarani ndani ya dakika kumi tu ntarudi nyumbani na nyama kilo tatu, vitunguu, mafuta, nyanya, karoti n.k

Mpendwa, nikikusimamisha nitakutafutia kosa lolote lile kwenye gari yako na hauwezi kuchomoka.Uzuri ni kwamba watu wa siku hizi hamtaki mambo mengi. Mnajifanya hamtaki kupoteza muda. Na hapo ndo MTAJI wangu ulipo.Naweza nikakusimamisha na kukuelekeza pa kuweka gari arafu nisikufuate.

Mwishowe eti utaona nakuchelewesha na ndipo utakapoamua kunifuata wewe mwenyewe na kunishikisha noti ya shilingi elfu tano ndipo nakuruhu uende huku nikijifanya kukusema kinafiki. Tazama, nalikamata basi la kwenda mkoani kwa kosa la mwendo kasi. Dereva ananikamatisha elfu tano namuachia aondoe ndinga.

Anaendelea na mwendo kasi, mara paah! ajali mbaya inatokea. Watu wanaaga dunia. Nikilala huwa nahisi zile roho zikinililia ila sijali chochote.

Tazama, nipo barabarani naongoza magari.Bosi mmoja ananipigia simu kwamba anataka kuwahi nyumbani, hivyo anataka nimvute. Unajua namvutaje?. Namvuta hivi, yeye ananiambia tu anatokea upande upi. Kwahiyo cha kufanya mimi nitasimamisha magari ya upande mwingine na kuyaita magari ya upande anaokuja nao yeye. Wakati mwingine naita magari ya upande husika hadi yanaisha, barabara inakuwa tupu, ila kwa kuwa mlengwa bado hajapita nitaendelea tu kuita magari ya upande huo hadi bosi kubwa apite. Baada ya hapo lazima ujumbe wa muamala utaingia kwenye simu yangu.

Kuna rafiki yangu yeye huvaaga zile SALE za MABAKA MABAKA. Yeye amenipa jina la MZEE WA KUKAMUA. Na ni kweli daladala nazikamua sana sana sana. Tena makondakta siku hizi sisi wakamuaji wametupa jina la TAKUKURU. Utasikia dereva anamwambia kondakta......"Oya usifungue mlango mbele kuna TAKUKURU''.

CHOCHOTE KITU:
Hiki ndicho kitu kinachofanya niipende kazi yangu na sijawahi kujutia kuifanya kazi hii, maana ninachoamini UTAMU WA KAZI NI PESA. Huu ni mwaka wa ishirini na saba nipo barabarani na sijawahi kukamatwa nikipokea chchote kitu.

Wapendwa, mwambieni MAMA kwamba, hakuna akili kubwa inayotumika kwenye kumkamua mwananchi wake mlala hoi. Mwambieni mbona hakuna usiri mkubwa sana kwenye kupokea kwangu. Mbona wakati mwingine nashikishwa ka elfu tano kangu huku abiria wakiona. Ila uzuri ni kwamba abiria na hata wapita njia wanaweza wakaona, ila taasisi yake ya kupambana na hili jambo haioni.

Tazama, nakunywa sana pombe. Nafanya sana zinaa na hasa na wake wa watu.Najua nilivyo mchafu.Nilishalazimisha wanawake watoe mimba zangu ambazo hadi Leo ni zaidi ya kumi.
Miaka miwili iliyopita niliwahi kuua mtu.
Hivyo najua nikifa leo nitaenda wapi. Roho yangu hainiambii kwamba eti nami ni wa peponi. Ni wazi moto na adhabu kali vinaningoja.

Mpendwa, kama na wewe una matendo kama yangu basi naamini ukifa utanikuta motoni nakusubiri.
Nasema utanikuta kwasababu naamini mimi nitatangulia na wewe utanifuata.

Mpendwa, ulishiriki kwenye kum bambikizia kesi mlala hoi asiye na hatia na akafungwa.

Ulidhurumu mali ya mnyonge kisa tu wewe una misuli ya nguvu ya fedha.

Ndugu wakili msomi. Unasimama mahakamani kumtetea mtu ambaye ni kweli ametenda kosa na pengine ameshakuambia ukweli kwamba ametenda. Ila wewe unamtetea kwa mbinu zako ili tu ionekane hajatenda kosa.

Mwenye nyumba,gari, shamba, kazi nzuri, unawasimanga wasio navyo na kuwaona takataka.

Tapeli wa mitandaoni. Mwizi. Unatangaza unauza bidhaa, baada ya kutumiwa fedha unam bloki aliyekutumia na bidhaa haumtumii.

Unakumbuka uliwahi kumnyima kazi mtu mwenye vigezo vyote hapo ofisini kwenu na badala yake ukamleta ndugu yako ambaye hakuwa kabisa na vigezo?.

Ulipewa pesa, ili ukatoe ushahidi wa uongo mahakamani.

Ulipewa pesa ili ukatoe ushuhuda wa uongo kanisani.

Daktari, muuguzi msaidizi, hauwajali wagonjwa masikini.Mgonjwa analetwa akiwa na hali mbaya sana, ila wewe upo tayari kama kufa afe tu kisa hana pesa ya kukuhonga ili apatiwe matibabu.

Wakunga hospitalini wenye matusi au maneno ya hovyo kuwaambia wajawazito.

Mpo wengi sana, sana, sana. Nyinyi hapo juu ni baadhi tu. Ila ZINGATIENI KWAMBA WENYE TABIA KAMA ZANGU AU KAMA ZENU HAPO JUU, NAWAAMBIA, HAKIKA MTANIKUTA MOTONI. Pengine naweza kuwa mwenyeji wenu mwema sana. Huko tutalia na kusaga meno.

NINI TUFANYE?.
Uzima ndio unaofanya nayaandika haya. Wewe unayasoma maandishi haya kwasababu na wewe una uzima. Kwahiyo sisi sote bado tupo hai. KWANINI WEWE UJE MOTONI NA UNIKUTE MIMI?. Hivi hatuwezi kubadilika ili tu tusikutane huko motoni?. Bado tunao muda. Tutubu dhambi zetu na tuanze maisha mapya.

JAMII HAIWEZI KUENDELEA KAMA KILA MTU KWA NAFASI YAKE ASIPOTIMIZA WAJIBU WAKE.

Mungu anibariki mimi na wewe ili tusikutane kweli huko kunakoitwa MOTONI.
Nimeipenda idea yako swahiba. Mimi ni miongoni mwa washiriki na andiko langu lenye kichwa Cha andiko "KILIMO CHENYE MANUFAA" . Niseme tuu uungwana ni kitendo una vote toka kwangu good idea.
 
Ongezea kidogo iwe riwaya isomwe mashuleni
 
Hongera mkuu kwa kutukumbusha makosa yetu
Makosa yetu wore mkuu. Kikubwa tubadilike tu. Kila mmoja atomize wajibu wake. Tuwe na hofu ya MUNGU. Tutende yampendezayo. Unajua binadamu anapokuwa anatenda jambo lisilo jema ni huwa anajua kabisa kwamba hili ninalotaka kulitenda siyo zuri. Ila ndo hilo hilo analitenda. Ila nafasi ya kutokutenda pia huwa IPO. Yatupasa kuing'ang'ania hiyo nafasi hata kama itakuwa nyembamba kama Uzi au unywele.
 
Back
Top Bottom