Ukifanikiwa kupata tobo la maisha ruksa kuwavimbia wabaya wako

Ukifanikiwa kupata tobo la maisha ruksa kuwavimbia wabaya wako

Moto wa volcano

JF-Expert Member
Joined
Jun 3, 2018
Posts
1,148
Reaction score
2,815
Maisha mpaka mtu kufanikiwa anakuwa amepitia mambo mengi kuna stages , kuchekwa , kupuuzwa , kusemwa vibaya , kudharauliwa .

Ukiona mtu ana roho mbaya haijaja bure amefundishwa na walimwengu wenyewe. Wanadamu ni wakatili sana kwa mtu asiye na kitu .

Ukifanikiwa kuyapata maisha vimba , Kuwavimbia walio kudharau ni ruksa kisheria . Ndioomaana hata Mungu aliwawekea kufuli waliomcheka na kumdharau Nuhu wakati anajenga safina , hakuna aliyeingia
 
Unaweza kuvimba hadi upasuke.
Tunapita tu ukipata vunga ishi kistaarabu.

Ombea adui yako waishi siku nyingi ili unapobarikiwa wajionee kwa macho,
Hamna haja kabisa afe kabla hajaona baraka ambazo MUNGU ameweka mbele yako.
 
Maisha mpaka mtu kufanikiwa anakuwa amepitia mambo mengi kuna stages , kuchekwa , kupuuzwa , kusemwa vibaya , kudharauliwa . ukiona mtu ana roho mbaya haijaja bure amefundishwa na walimwengu wenyewe. Wanadamu ni wakatili sana kwa mtu asiye na kitu . Ukifanikiwa kuyapata maisha vimba , Kuwavimbia walio kudharau ni ruksa kisheria . Ndioomaana hata Mungu aliwawekea kufuli waliomcheka na kumdharau Nuhu wakati anajenga safina , hakuna aliyeingia
ni kweli mafanikio yana mlolongo mrefu sana lakini hilo la kuwavimbia watu mi nalikataa maana kesho yako huijui, jifunze kuwa mnyenyekevu hata kama maisha umeyapatia kwa sababu kuna kufilisika na kuumwa hao unaowavimbia kuna siku usioijua utahitaji msaada wao
 
Mapicha picha ya kujitafuta yalivyo ya kutisha. Nah! bro Acha watu wavimbe.

Picha linaanza Kwanza MTU anazeeka akiwa anajitafuta, Akijipata ndo ujana unaanza kumtafuta
Hapo amesha kutana na K.O za kila Aina ya Changamoto .

Kuvimba muhimu kikubwa kuvimba kwa plans .
 
ni kweli mafanikio yana mlolongo mrefu sana lakini hilo la kuwavimbia watu mi nalikataa maana kesho yako huijui, jifunze kuwa mnyenyekevu hata kama maisha umeyapatia kwa sababu kuna kufilisika na kuumwa hao unaowavimbia kuna siku usioijua utahitaji msaada wao
Unakuta hayo yote mtu aliyapitia na bado hao watu hawakumuonesha sympathy zaidi ya kumcheka
 
Maisha mpaka mtu kufanikiwa anakuwa amepitia mambo mengi kuna stages , kuchekwa , kupuuzwa , kusemwa vibaya , kudharauliwa .

Ukiona mtu ana roho mbaya haijaja bure amefundishwa na walimwengu wenyewe. Wanadamu ni wakatili sana kwa mtu asiye na kitu .

Ukifanikiwa kuyapata maisha vimba , Kuwavimbia walio kudharau ni ruksa kisheria . Ndioomaana hata Mungu aliwawekea kufuli waliomcheka na kumdharau Nuhu wakati anajenga safina , hakuna aliyeingia
kuvimba hapana, ila wafungie vioo yaani hakikisha wakujue undani wa mafanikio yake tena yaani hakikisha wanaishia kukujua enzi ukiwa fukara bac.
 
Back
Top Bottom