Ukifika The Centro de Treinamento George Helal, punguza mwendo, toa heshima endelea na safari zako

Aaron Arsenal

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2014
Posts
24,501
Reaction score
28,711
Ufikapo Jiji la Pwani Rio de Janeiro, au 'River of January' jiji la pili kiuchumi nchini Brazil baada ya Sao Paulo, limepakana na milima pamoja na bahari ya Atlantic, mji huu upo chini ya Governor Wilson Witzel YES, takribani watu 16 million wapo hapo.

Anyway sisi hatuna sana issue na mambo yao, ila sisi tunaelekea mitaa ya Vargem Grande magharibi mwa Rio de Janeiro, moja kati ya mitaa yenye sifa kama Manzese ya Dar Es Salaam, kwa wahuni na watukutu wakubwa sana.

Mitaa hiyo ndipo maskani ya klabu kubwa nchini humo, Club De Regatas do Flamengo 'Flamengo' inayotumia dimba la Maracana kukiwasha mechi zake, turejee nyuma kidogo Agosti 30, 1984 Rais George Helal alinunua kiwanja kikubwa ili kuweka miradi mbali mbali ya klabu ya Flamengo.

Wazo lake liliishi kichwani mwake, wakapita wakina Zico, Ronaldinho Gaucho, Romario, Zizinho bila kushuhudia au kuliishi wazo lake ila 2011 Rais mpya aliona iko namna ya kutengeneza Academy ya soka na miundombinu ya kimichezo kwa ajili ya Flamengo.

Mjengo ulianza kujengwa 2011 na kukamilika 2012, wakaanza kuutumia ila 2016 ulirekebishwa tena ili kutumika kwenye Olympics, zikaongezwa Medical center, press room na pitch nyingi zaidi.

Wakati Brazil wakiimba utukufu wa klabu hiyo kongwe, wenyewe wakaamua kupaita makao makuu kama George Helal Training Center kwa heshma ya Rais wao wa zamani

Ila wahuni kutokea mitaani wakapaita Ninho du Urubu 'The Vultures Nest' hii ni nyumba ya tai YES uliwahi kufahamu kwanini? Wao wenye wahuni kutokea mitaa hiyo waliamini kuwa ndani mle kuna mafundi wanaishi, ndani mle kuna watu wamezaliwa kwa ajili ya soka tu, wamezaliwa kwa ajili ya kuwatesa wenzao, wakiamini kuna mastraika na viungo wa hatari wenye uwezo wa kupiga vyenga kiasi cha kutegua watu viuno

Hao ndo Wabrazil na utamaduni wao, wenyewe wanaamini unapokaribia mitaa hiyo, basi punguza mwendo geuka salimia kasri la soka, salimia sehemu aliyopita Dinho wa Gaucho na Brazil football wizard Zico, geuka mpe salamu Romario.

Karibu Ninho du Urubu, karibu Rio De Janeiro, Pwani ya soka iliyojigeuza Manzese ya Dar Es Salaam, mambo mengi muda mchache[emoji119]

 
Sawa mwana Gunnerz mwenzangu.
 
Brasileiras

Mpira unaipenda Brazil aisee
 
Huyu mshkaj Ronaldinho..yaan alifanya mpira uonekane mwepesi sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…