Ni kwamba tu dini hizi zilianzishwa zamani sana ndiyo maana tunaona sawa. Mimi ni mkristo, lakini leo atokee Seremala aanze kusema ni mwana wa Mungu na katoka mbinguni lazima kila mtu ashtuke na kumuona hayupo sawa kichwani...
Mkuu, ni hivi, tangu zamani kulikuwa na namna ya kuwachuja manabii, na hata leo maelekezo yapo jinsi ya kuchuja uongo na ukweli.
usipo kuwa mwerevu na unayejua mambo ya Mungu utadanganyika. ni rahis kupotezwa.
Hivyo alipotokea mtu akadai ni nabii au mtume alipimwa. Hata zumaridi anatakiwa kupimwa kwa vigezo na kuwekwa kunakostahili
Kumbukumbu 13:1-3 “Kukizuka katika yako nabii, au mwotaji wa ndoto, akikutolea ishara au ajabu, ikatukia hiyo ishara au hiyo ajabu aliyokuambia, akisema, Na tuifuate miungu mingine usiyoijua, tuitumikie hiyo; wewe usiyasikilize maneno ya nabii yule, au yule mwotaji wa ndoto…”
Kutokana na andiko hili hapa juu linaonyesha wazi ya kwamba tunaweza kuwatambua manabii wanaopotosha kwa mambo yale wanayotuambia au kutuelekeza kinyume na neno la Mungu. Na ikiwa hawana matunda mazuri hao ni manabii wa uongo. Ndio maana imeandikwa; Mathayo 7:15-20 “Jihadharini na manabii wa uongo, watu wanaowajia wamevaa mavazi ya kondoo, walakini kwa ndani ni mbwa - mwitu wakali. Mtawatambua kwa matunda yao. Je! watu huchukua zabibu katika miiba, au tini katika mibaruti? Vivyo hivyo kila mti mwema huzaa matunda mazuri; na mti mwovu huzaa matunda mabaya Mti mwema hauwezi kuzaa matunda mabaya, wala mti mwovu kuzaa matunda mazuri. Kila mti usiozaa tunda zuri hukatwa ukatupwa motoni.
Ndiposa kwa matunda yao mtawatambua.” Mfano wa mti mwema ni yule mtu anayeyafanya mapenzi ya Mungu (matakwa ya Mungu). Na mfano wa mti mwovu ni mtu asiyeyafanya mapenzi ya Mungu.
7.Unabii walioutoa ulilingana na neno la Mungu. Haukupigana na neno la Mungu mahali popote katika biblia. Mwamini anaweza kuutambua unabii kwa kutumia neno la Mungu. Lakini ni lazima kwanza ayafahamu maneno ya Mungu na kuyahifadhi moyoni.
Wakolosai 3:16
"Na neno la Kristo na likae kwa wingi ndani yenu katika hekima yote…” Mtu akiwa na maneno ya Mungu kwa wingi moyoni anaweza kuyapima mambo yote ya Kiroho.
Jinsi ya kuwatambua manabii wa uongo. Ni kwa njia zifuatazo;
1. Tunaweza kuwatambua au kuwapambanua kwa tabia zao ambazo haziendani na neno la Mungu na ziko dhahiri wala haziwezi kufichika. Tunaweza kuwatambua kwa kutumia neno la Mungu na tunda la Roho.
Wagalatia 5:22-23.
“Lakini tunda la Roho ni upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu, upole, kiasi; juu ya mambo kama hayo hakuna sheria.”
2. Kuwatambua kwa mafundisho yao ya kibinadamu. Mafundisho yao wameyatunga hayaendani na neno la Mungu. Wanafundisha na kuhubiri kwa kutafsiri mistari ya biblia kinyume neno la Mungu. Kwa sababu hiyo wanakuwa wamewapotosha waamini katika njia ya Mungu. Hutumia mafundisho ya uzushi na uongo na kuyachanganya na maandiko ya neno la Mungu kana kwamba ni neno la Mungu. Kwa sababu hiyo huwapotosha wasiolijua neno la Mungu kwa ukamilifu. Ikiwa mwamini yuko makini na anayafahamu maandiko kwa ukamilifu ni lazima atagundua ya kwamba mafundisho wanayofundisha na kuyahubiri yanapingana na neno la Mungu katika biblia. Ndio maana imeandikwa tusiamini kila roho (kila nafsi) tuzijaribu kwanza. 1Yohana 4:1.
“Wapenzi msiiamini kila roho, bali zijaribuni hizo roho, kwamba zimetokana na Mungu; kwa sababu manabii wa uongo wengi wametokea duniani.”
Kujua maandiko ni muhimu sana