Ukifuata muongozo huu wa kukaa kimya unastahili kheri ya mwaka 2021

Ukifuata muongozo huu wa kukaa kimya unastahili kheri ya mwaka 2021

comte

JF-Expert Member
Joined
Dec 11, 2011
Posts
9,019
Reaction score
6,825
WAKATI MWINGINE KAA KIMYA:
1. Kaa kimya unapokuwa na hasira.
2. Kaa kimya unapokua huna uhakika wa unachokitetea.
3. Kaa kimya unapokuwa hujathibitisha ukweli wa unachotaka kukisema.
4. Kaa kimya kama maneno yako yataleta maudhi.
5. Kaa kimya wakati ambao unapaswa kusikiliza.
6. Kaa kimya pale ambapo unataka kukejeli au kudhihaki mambo ya kweli.
7. Kaa kimya kama hilo suala halikuhusu.
8. Kaa kimya kama unaona utalazimika kusema uongo.
9. Kaa kimya kama unajua kuwa maneno yako yataharibu au kuumiza hadhi ya mtu.
10. Kaa kimya kama maneno yako yataharibu urafiki wenu.
11. Kaa kimya kama nia yako ni kupinga tu.
12. Kaa kimya kama maneno yako yatamuaibisha Mungu au familia yako.
13. Kaa kimya kama unajua kuwa unaweza kuyajutia maneno yako baadae.
14. Kaa kimya kama umeshazungumza tena na tena juu ya jambo hilo na hakuna kinachobadilika.
15. Kaa kimya kama unatakiwa kuwa bize na shughuli zako.
 
Back
Top Bottom