KERO Ukifungua RB Arusha Central Police jiandae kujigharamikia huduma za stationery

KERO Ukifungua RB Arusha Central Police jiandae kujigharamikia huduma za stationery

  • Thread starter Thread starter Anonymous
  • Start date Start date
Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Kituo Kikuu cha Polisi cha Kati Arusha ukipeleka malalamiko unataka kukata RB, wanakwambia “Karatasi ya kunukuu maelezo hatuna” kisha wanakupa moja wanakwambia katoe kopi tano ulete na ukanunue na faili la jalada.

Wakati wanakwambia hivyo wanakupa maelekezo ya kwenda Stationary ipo jirani ambapo kuto copy ni Shilingi 200.

Huu ni uonevu, mlalamikaji huchukuliwi maelezo mpaka ukalete kopi na faili, inamaana Serikali haihudumii vitu kama hivi au ni upigani ambao unafanyika ili hiyo Stationary ifanye biashara?
 
Kwako RC Paul Christian Makonda.

Kwa kituo kama hicho kinahitaji Photocopier Machine, Chumba Cha Stationeries, pamoja na Kitengo Cha IT kuwahudumia walipakodi walalamikaji.
 
Kituo Kikuu cha Polisi cha Kati Arusha ukipeleka malalamiko unataka kukata RB, wanakwambia “Karatasi ya kunukuu maelezo hatuna” kisha wanakupa moja wanakwambia katoe kopi tano ulete na ukanunue na faili la jalada.

Wakati wanakwambia hivyo wanakupa maelekezo ya kwenda Stationary ipo jirani ambapo kuto copy ni Shilingi 200.

Huu ni uonevu, mlalamikaji huchukuliwi maelezo mpaka ukalete kopi na faili, inamaana Serikali haihudumii vitu kama hivi au ni upigani ambao unafanyika ili hiyo Stationary ifanye biashara?
Siyo Arusha tu hata Morogoro naona kuna utaratibu huo
 
Ni Kweli la siku nyingi Hilo nimewahi kuwa na kesi ktk kituo hcho

Hat loss ripoti inakubidi akote kopi na hat Kama zimejah karatasi mezani

Kituo Cha Police nikama kichaka tu
 
Tanzania bado tuko enzi za ujima, kwanza makaratasi ya nini kwa dunia ilikofika?
 
Ni tabia ya polisi nchi nzima. Na faili ni yale majaladio ya daftari la wanafunzi wa primary yale ya kaki
 
Kwa ufupi JESHI letu la POLICE ni shida..usiombe uibiwe,yaani yule MPELELEZI auto anakuwa mtoto wako wa HIYARI..wengi huwa tunaamua kuacha tu..ila ni KERO sana hao watu
 
Pesa wanatumia kwenye Mwenge au kununua hayo magoli ya kwenye mpira yangemaliza kabisa tatizo ya stationary kwenye vituo vya polisi kote Tanganyika.
 
Back
Top Bottom