Ukigeuka mshauri kwenye mahusiano yako jua upo unalazimisha afanane na unayemtaka, tayari umechanganya mafaili

Mwanasayansi Kalivubha

JF-Expert Member
Joined
Feb 4, 2024
Posts
344
Reaction score
926
Kuelimishana ni muhimu kwenye mahusiano ila ukiona kila siku unakuwa mshauri kwake jua upo unamlazmisha afanane na unayemtaka.

Kwenye mahusiano kuna kukosea vigezo baadhi na kukosea vigezo vingi kwenye machaguo, aliyekosea vigezo baadhi huyu ni rahisi kujifunza kuvumilia ila kwa aliyekosea sana mara nyingi hujikuta kwenye zoezi la kumbadilisha ili awe yule anayemtaka zoezi ambalo linashinda wengi.

Ukiona toka mapema unatumia nguvu kubwa kumshauri awe yule unayemtaka ukiweza fanya maamuzi magumu kwa sababu hilo zoezi ufaulu wake upo kwa wachache sana ila wengi wanafeli.

Pia soma: Nimeachwa na mtu ninayempenda sana, nimeshindwa kukubaliana na hali

Utakuwa unamshauri kila siku abadilike kufanana na unayemtaka ila kadri ufanyavyo hivyo ndivyo na yeye anazidi kuwa vile alivyo na matokeo yake mtaaanza kukorofishana kila siku kwa sababu ki asili binadamu hapendi kubadilishwa.

Ki asili binadamu hapendwi kubadilishwa bali ajibadilishe mwenyewe hivyo akiona una lengo la kumbadilisha ataanza kukuchukia na kukukwepa.

#FIKIA NDOTO ZAKO.
 
UKIGEUKA MSHAURI KWENYE MAHUSIANO YAKO JUA UPO UNALAZIMISHA AFANANE NA UNAYEMTAKA, TAYARI UMECHANGANYA MAFAILI 😔

Kuelimishana ni muhimu kwenye mahusiano ila ukiona kila siku unakuwa mshauri kwake jua upo unamlazmisha afanane na unayemtaka.

Kwenye mahusiano kuna kukosea vigezo baadhi na kukosea vigezo vingi kwenye machaguo, aliyekosea vigezo baadhi huyu ni rahisi kujifunza kuvumilia ila kwa aliyekosea sana mara nyingi hujikuta kwenye zoezi la kumbadilisha ili awe yule anayemtaka zoezi ambalo linashinda wengi.

Ukiona toka mapema unatumia nguvu kubwa kumshauri awe yule unayemtaka ukiweza fanya maamuzi magumu kwa sababu hilo zoezi ufaulu wake upo kwa wachache sana ila wengi wanafeli.

Utakuwa unamshauri kila siku abadilike kufanana na unayemtaka ila kadri ufanyavyo hivyo ndivyo na yeye anazidi kuwa vile alivyo na matokeo yake mtaaanza kukorofishana kila siku kwa sababu ki asili binadamu hapendi kubadilishwa.

Ki asili binadamu hapendwi kubadilishwa bali ajibadilishe mwenyewe hivyo akiona una lengo la kumbadilisha ataanza kukuchukia na kukukwepa.

#FIKIA NDOTO ZAKO.
True 100%
 
Back
Top Bottom