Ukiiangalia vizuri dunia ni kama imesimama

Uwesutanzania

JF-Expert Member
Joined
Feb 9, 2019
Posts
1,380
Reaction score
1,686
Ni mimi wako UWESUTANZANIA ✍️

Naam imesimama,

Namaanisha imesimama kiteknolojia na ugunduzi na utatuzi wa changamoto za binaadam za kila siku.

Ukisoma vitabu Dunia wakati inaumbwa haikuwa na (magari, pikipiki, saa, simu, radio, tv, engine, cherehani, nk.

Bali aliumbwa adam na hakupewa elimu ya namna ya kutatua changamoto zake za maisha ya kila siku.

Lakini cha ajabu na kushangaza ni kuwa hivi vitu vyote vilivyo leo hii ni kama pia vililetwa siku moja. Yaani (magari, pikipiki, saa, simu, radio, tv, engine, cherehani, nk.

Adam hana muendelezo tena (DUNIA IMESIMAMA) bali akili yake imeishia kwenye kuboresha na kuendeleza vile vile ambavyo katika historia vimo humo tokea miaka ya 1600s. Sina hakika alivigundua kweli kwa akili yake au Lah. Maana sioni tena matumizi mapya ya akili yake.

Hata ukichukuza bidhaa zinazozalishwa viwandani ukilinganisha vya zamani na vya sasa utagundua kuwa vya zamani vilitengenezwa kwa ubora na uimara wa hali ya juu.

Je ugunduzi wa project mpya ulifia wapi?
Au ni kweli kuna mahusiano ya moja kwa moja na viumbe vya sayari ya mbali?

Nb* kwenye bandiko langu nazingumzia vitu vipya na vifaa vipya, yaani kuwepo na ugunduzi hata wa vyanzo vya nishati vipya bila ya kuhusisha vyombo vya zamani,. Yaani gundua vitu bila kuhusisha engine, waya, petroli na dizeli, nk.
 
Me sijaelewa unazungumzia hakuna ugunduzi wa vifaa vipya au nishati mpya tokea lini 1600s au 1960s,
 
Mkuu ungeweka time frame.... ugunduzi uliishia wakati gani haswa?
 
zama za mawe za kati za kale za enzi
Mkuu zama za mawe ni zamani sana aisee, enzi hizo binadamu ndio kwanza alikua anaanza kujua ku adapt kwa kuanza kujua kuhusu mazingira na vitu vinavyo mzunguko ili kuvitumia kwa manufaa..... just imagine anatumia jiwe kama kisu?

Nadhani (sina hakika)zama za mapinduzi ya viwanda ndio era ilikuja kuwa na gunduzi nyingi sana ambazo ndio msingi wa maendelo ya kisayansi na teknolojia tunayo boresha sasa
 
Kugundua kitu kipya ambacho hakijawahi kuwepo huo sio ugunduzi huo ni uumbaji ishi humo.
Sidhani kama ni kweli, we fikiria tarehe moja mwezi wa kwanza mwaka moja, je simu ya mkononi ilikuwepo? kwahio ilivyogunduliwa miaka kadha wa kadha baadae ndio tuseme iliumbwa, au ulimaanisha kuunda mkuu? mleta mada kamaanisha gunduzi mpya, yani mfano leo hii ugundue lugha ambayo itaeleweka na binadamu wote duniani bila kufundishwa wala kufasiliwa.
 
Naam kabisa. Umenielewa vizuri mkuu
 
Mkuu zama za mawe ni zamani sana aisee, enzi hizo binadamu ndio kwanza alikua anaanza kujua ku adapt kwa kuanza kujua kuhusu mazingira na vitu vinavyo mzunguko ili kuvitumia kwa manufaa..... just imagine anatumia jiwe kama kisu?

Nadhani (sina hakika)zama za mapinduzi ya viwanda ndio era ilikuja kuwa na gunduzi nyingi sana ambazo ndio msingi wa maendelo ya kisayansi na teknolojia tunayo boresha sasa
Na kwanini tuendelee kuboresha tu na kusiwe na gunduzi mpya
 
Nadhani kwa sasa mambo mengi yaliyokwisha gunduliwa yanampatia binadamu karibu kila kitu kinachowezekana na kumfanya awe mvivu
Sana sana anafanya maboresho tu

Lakini pia kuna nadharia kwamba zipo gunduzi nyingi lakini zinawekwa “kapuni” kwasababu zitaharibu biashara za watu na uchumi wa nchi kubwa
 
Sidhani kama ni kweli, we fikiria tarehe moja mwezi wa kwanza mwaka moja, je simu ya mkononi ilikuwepo? kwahio ilivyogunduliwa miaka kadha wa kadha baadae ndio tuseme iliumbwa, au ulimaanisha kuunda mkuu? mleta mada kamaanisha gunduzi mpya, yani mfano leo hii ugundue lugha ambayo itaeleweka na binadamu wote duniani bila kufundishwa wala kufasiliwa.
Huwezi kugundua kitu kipya kwa sasa hivi coz vyote vya msingi vimeshagunduliwa labda uumbe.
 
Dunia bado kuna changamoto nyingi za kibinaadamu.

Mfano upepo.

Dunia inahitaji ugunduzi wa vidhibiti upepo na vimbunga.

Pia vidhibiti vya tetemeko la ardhi kama ilivyo kwenye radi.

Pia tunahitaji vileta mvua yaani unawasha kifaa wingu linafunga na mvua inanyesha ukiona inatosha unafunga.

Kuna changamoto pia kwenye uzazi,.

Gunduzi inahitaji kumsaidia mama mjamzito ukiachana na visu inayoleta athari kubwa.

Kwenye uzazi wa mpango pia kuna shida, njia zote zinazotumika na dunia ya sasa hivi sio salama bado tunahitaji gunduzi mpya zaidi.

Kwenye nishati nako bado changamoto tunahitaji vyanzo vingine ukiachana na jua, maji, mafuta (dizeli na petrol), makaa ya mawe na upepo.

Kwenye uhai bado na kwemyewe kuna changamoto dunia inahitaji ugunduzi na utatuzi wa kufanya maisha yawe endelevu kidogo hata miaka 250nk.

Kwenye magonjwa pia kuna changamoto kuna h
itaji gunduzi ya haraka (UKIMWI, KANSA nk
 
Anza wewe mkuu usitutupie kila kitu sisi.
 
Back
Top Bottom