UKIIGA KITU KIZURI, HUFI!

UKIIGA KITU KIZURI, HUFI!

Efendi

JF-Expert Member
Joined
Aug 23, 2016
Posts
314
Reaction score
438
Simba SC wanatufundisha kuwa; kuna Afisa Habari(Media Officer) hapa amelengwa Gift Macha na pia atakuwepo Msemaji wa Klabu(Club Spokerman) hapa anabaki Sheikh Haji Manara(sijui imeeleweka hii).

Sasa twende sawa.... Yanga woooote geukieni huku tulijue hili. Kwa wanachokifanya Simba SC kwa sasa ni kuwaonyesha Yanga Sc makosa yao ya sasa. Kwa maana ya Yanga wanataka kumuondoa Afisa Habari D10 ili wampate Msemaji wa timu mwenye Kaliba ya Haji.

Yawezekana kabisa, Simba Sc walitamani sana kuwa na Afisa Habari wa kaliba ya Dismas Ten(D10).... Ndio kaliba ya D10 ambaye wanaYanga wanamtaka afungue mlango awaachie chumba chao Habari pale Jangwani sababu ameshindwa kuwa Msemaji wa Timu na kubaki kuwa Afisa Habari tu.

D10 ni mbunifu(creative) sana na ndio maana halisi ya afisa habari. Gift atakwenda kwa mfano wa anachokifanya D10 pale Yanga(Wanayanga endeleeni kugeukia huku), Pale Yanga kuna Yanga TV, press conference room tunaiona na mambo mengi ambayo yameongezwa na ubunifu wa D10 kwa ubunifu maridhawa.

Sasa kazi kuubwa anayokwenda kuifanya Gift pale Simba Sc ni ile ambayo haikufanywa na Haji Manara kwa asilimia kubwa. Ila Haji anabaki kwenye eneo maridhawa analolimudu la Usemaji wa Timu(Hapa nimewaelewa Simba Sc bila hata kunywa kahawa).

Ndio..! Kuna angle ambazo D10 anamzidi Haji Manara(hapa ni katika idara ya Afisa Habari), ila pia kuna eneo ambalo D10 hamsogelei Sheikh Haji Manara hata chembe(hapa ni katika Usemaji wa Klabu).

Yanga geukieni huku walipo Simba SC, kuna chakujifunza huku. Haji yupo na umahiri wake pale pale(Usemaji) ila Simba walikuwa wanamkosa D10 ambaye idara yake ya Uafisa habari.

Sasa Yanga mnahitaji Msemaji wa timu tu maana Afisa habari teyari tunae.

Ukiiga kitu kizuri HAUFI kamwe.
 
Lini yanga walisema wanataka kumtoa D10? Mambo ya mitandao usiifanye rasmi ukizingatia mnaianzisha wenyewe na kuipromote.
 
Sasa msemaji wa team ya 5imba mbona huwa anaisema Yanga?

hebu fafanua hapo mwana mbumbumbu fc aka mikia fc ili vyura fc aka ndala fc wakuelewe
 
kwa hiyo kazi msemaji wa simba Manara ni kuitukana Yanga, Mbumbumbu bana hakuna msemaji wa timu yoyote hapa duniani mpumbavu kama manara
 
Back
Top Bottom