GoldDhahabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2023
- 7,189
- 10,375
Inasemekana, ubinafsi ni sababu mojawapo inayowapelekea watu wengine kujinyonga. Ni Kwa sababu ya kujifikiria zaidi kuliko wanavyowafikiria wengine.
Kadiri mtu anavyojifikiria sana, kwa wengine, ndivyo wanavyojiona hawafai au hawana faida. Lakini kama angefikiria jinsi ya kuwasaidia wengine, kungemsaidia kujisahau na mapungufu yake, na hivyo msongo wa mawazo kumwacha.
Inasemekana, hata baadhi ya wagonjwa wanaolazwa mahospitalini kwa sababu ya msongo wa mawazo, wasingeifikia hiyo hali kama wangejizoesha kuwawazia wengine mema, tena mema tu.
Daktari mmoja aliwaelekeza wagonjwa wake waliokuwa wakisumbuliwa na msongo wa mawazo kuhakikisha kuwa kila siku wanamtendea mtu mmoja jambo litakalomfurahisha. Matokeo yake, kila mgonjwa aliyefuata huo ushauri alipona ndani ya wiki moja.
Imeandikwa, kutoa ni bora kuliko kupokea. Hakuna asiye na kitu cha kutoa, kama si mbinafsi. Tabasamu lake pekee linaweza likawa msaada mkubwa kwa mwenye uhitaji huo. Kauli yake moja ya kutia moyo inaweza ikatenda muujiza kwa mpokeaji. Ikiwa alikuwa akimfukiria mhusika kiusahihi, atajua cha kusema kitakachoweza kumsaidia.
Inasadikika kuwa miongoni mwa watu wenye furaha sana ni wale waliochagua kuishi kwa ajili ya kuwasaidia wengine.
Nicholas James Vujicic, ni mmoja wa "motivational speaker" maarufu duniani. Ingawa alizaliwa akiwa hana miguu wala mikono, anafanya kazi ya kuwatia moyo na kuwahamsisha watu kwa mema. Hajauruhusu ulemavu wa miguu na mikono aliozaliwa nao kuingia moyoni mwake. Hajioni mlemavu kwa sababu ameuchagua kujiona vinginevyo. Haishi kwa ajili ya kusaidiwa bali kusaidia wengine. Na inasemekana, Nicholas ni mmoja wa matajiri wanaotia misaada ya kuwasaidia wahitaji.
Kwa hali yake ya ulemavu, asingechekwa kama angeamua kuwa omba omba. Lakini Nicholas aliamua kuwa mtunwa kusaidia na siyo wa kusaidiwa.
Stanford university ni miongoni mwa Vyuo Vikuu maarufu nchini Marekani. Kilianzishwa na Stanford mwaka 1885 baada ya kumpoteza mwanaye wa pekee, Leland Stanford Jr, mwaka 1884 kwa ugonjwa wa typhoid.
Muda mfupi baada ya mtoto wake kuaga dunia, alimwambia mke wake, "Watoto wa California watakuwa watoto wetu". Ni huo mtazamo ndiyo uliomchochea kukianzisha Chuo cha California. Hakukijenga kwa lengo la kujipatia umaarfu, bali aliwajengea "watoto wake". Lakini mpaka leo, ingawa alishaaga dunia miaka mingi, bado watu wanaukumbuka wema wake.
Watangulize wengine katika mambo mema. Hata ikibidi, kuwa baba au mama kwa "yule" mtoto mwenye uhitaji huo.
Kuna faida tele katika kuisahau nafsi yako na kuchagua kuwatanguliza wengine. Inalipa sana.
Ukiamua kujisahau kwa manufaa ya wengine, wengine watakukumbuka daima!!!