Ukiistaajabu ya Job Ndugai utayaona ya TEC

Ukiistaajabu ya Job Ndugai utayaona ya TEC

The Burning Spear

JF-Expert Member
Joined
Dec 23, 2011
Posts
4,118
Reaction score
9,864
Watanzania tumekuwa wagumu sana wa kujifunza kutokana na historia, nakumbuka namna job ndugai alivyokodishiwa wahuni kumtukana na mpaka kujiuzulu kisa kasema nchi inauzwa, tumekuja kugundua badae sana maana ya kauli yake.

Hata huku kusakamwa kwa TEC wala sishangai ni akili za watanzania za kushikiwa, CCM hawapendi kuambiwa ukweli hata kidogo, na huwa wanatumia kila mbinu kumdhoofisha mkosoaji wao, watanzanaia ifike mahali tujifunze CCM inapotumia nguvu nyingi kunyamazazisha jambo mjue kuna jambo jeusi linaendelea kwa nyuma yake, TEC hawajaanza leo kutoa waraka Tanzania huu ni utamaduni wao.

Nimejaribu kufuatilia ujumbe wa TEC Umekuwa ni mwiba mkali sana hasa kwa wenye ajenda zao binafsi juu ya uwekezaji wa bandari, hadi samia anaanza kwenda kutafuta huruma huko kwenye makanisa ya kilokole, naye Kikwete kakimbilia kwa wasabato huko rorya kutia huruma maana walijua kabisa kuna waraka unakuja.

Ikumbukwe kabla ya waraka wa TEC kuna nyaraka nyingi zilishatoka kama za TLS, kamati ya bunge , Chadema nk Lakini hapakuwa na nongwa yoyote, ukisoma nyaraka zote zilizotoka hazina tofauti kubwa sana zote zinaongea mambo yale yale. Je, Inakuwaje waraka wa TEC ushambuliwa? CCM mnahofu gani wakati waliotoa waraka ni watnzania wenzenu wanaotaka maslahi ya nchi yalindwe na hawajatokea Burundi.

Kama Samia ameamu kuwagawanya nayi mmeamua kugawanyika kazi kwenu, CCM Itaendelea kuwanyoa upara klla siku.
 
Back
Top Bottom