Ukikosa location sahihi ya biashara yako bora usifungue hiyo biashara

CHASHA FARMING

JF-Expert Member
Joined
Jun 4, 2011
Posts
7,872
Reaction score
9,263
Moja ya vitu vinavyo hitaji umakin wa kiwango cha juu kabisa ni location.

Na hii ndo sehemu watu wengi huwa hawaizingatii kabisa, Location ina mchango mkubwa mno kwenye kuimarisha biashara ya mtu.

Sasa utashangaa watu sijui huwa wanalazimishwa au hawana namna mtu anafungua biashara yake location ambayo unabaki kujiuliza maswali.

Ukikosa location sahihi bora usifungue biashara hiyo weka pesa benki au basi hakikisha biashara yako ina wateja maalumu.

Biashara nyingi zinazo fungwa sababu kubwa huwa ni location. Ni ngumu sana kuwa na location sahihi then ufunge labda uwe umekula mtaji.

Huwezi mfano kufungua mgahawa wa Chakula pale Kariakoo then ufunge labda uwe umeibiwa pesa yote ya mtaji, au mwenye nyumba anataka kubadilisha matumizi. Pale lazima watu wale tu.

Location zinaumiza sana watu na wengi hawazingatii kabisa hilo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kweli kabisa, wakati mwingine mtu anaamua tu afungue biashara kwakua ana mtaji wa kufanya hivo bila kushirikisha factors nyingine, mwisho ni kuangukia pua.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
WANAKUJA KUKUPA MWONGOZO MKUU!!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
. Location ndio biashara yenyewe mkuu, ukifeli hapo ata uanze na mtaji wa mamilion utakwama tuu na mtaji utapotea.
 
True

Kuna jamaa alifungua sehemu ya huduma za gari yaani Carwash, duka za spare na servive eneo kubwa kajenga kisasa roundly uwekezaji unafika 30MIL ila nilivyoona investment husika na location nikasema hapa kaenda chaka kweli biashara sasahivi ukipita imekufa wamevunjavunja ijafika hata nusu mwaka.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
NBC alikuwa na tawi Kinondoni manyanya na BACLAYS Kinondoni karibu na Muslim, but wote chali! na hapa tuseme tatizo location?
 
Location nzuri zote zina watu na hata kama Ukiipata Bei yake mkasi

Kuna mtu mmoja humu aliwahi kusema Haijalishi uko location gani kama hufanyi matangazo ni kazi bure tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…