Imenikunbusha November mwaka jana tukiwa kwenye BM tunatoka Arusha kuja Dar, mama mmoja alimwachia mwanaye wa miaka kama 5 hivi simu acheze games, tukiwa mitaa ya Mbwewe kuitafuta Wami mama mtu akapitiwa usingizi, kitoto kikahama siti kikakaa siti ya nyuma yake na kuanza kutazama video, baadaye tunasikia clip zinatoa miguno ya porns, mama mmoja mtu mzima wa kama 40s+ akawa naye amekodoa macho anatazama baadaye akainuka bwana mmoja akapokonya ile simu akamfuata yule mama mwenye mtoto na kumwambia afute clip zote vinginevyo anamfungulia mashitaka.