Ukikutana na changamoto hii utafanya nini?

Kali _D

Senior Member
Joined
Feb 10, 2019
Posts
145
Reaction score
132
Mara Paaaap.. Umerudi zako home Unakuta Panya 6 (sita)
1. Panya wa kwanza anakula MsaaFu au Biblia
2. Panya wa Pili anakula Cheti cha Degree
3. Panya wa Tatu anakula Hati ya Nyumba
4. Panya wa Nne anakula Viza ya Kusafiria
5. Panya wa Tano anakula Cheti cha Ndoa
6. Panya wa Sita anakula Cheki ya Milioni 100

Swali Ni:
Je! Utaanza kumuua Panya yupi?
.......
Sema ukweli aseee Rafiki
 
Mi naokoa kwanza hiyo check maan a hiyo hela inaweza rudisha hivyo vingine
 
Nawaletea paka 6 watapambana nao.


Ndukiiiii 🏃‍♂️🏃‍♂️🏃‍♂️
 
Mbona hivyo vyote ni.vya kupita tuu. Vinaweza kupatikana tena so dawa ni kuyaondoa wote Ile next time wasilete uharibifu
 
Obviously milioni 100 inaweza kuleta hivyo vingine vyote so I will deal with #6. Ila umeandika utoto sana shwaini
 
Hao panya watakuwa wanajua kusoma? Kwanini wafuate hivyo vitu tu? Au hivyo vyeti/misahafu/hundi navyo vinatunzwa stoo?
 
Huyo anayeitafuna biblia nitamuua haraka mno….mengine hayo yatafuata
Sisi binadamu tuna vituko sana. Panya ni kiumbe cha MUNGU, amekiumba akakiamuru ili kiweze kuishi basi kile hata karatasi. Wewe unakiua sababu kimekula karatasi halafu utasema umekiua kumtetea MUNGU au neno lake . Kesho wakitokea wa imani tofauti wakachinja watu sababu ya kitabu Chao unawaona ni mashetani. Sasa hapo mna tofauti gani? Wote wauaji tu mnatoa roho za viumbe visivyo na hatia.
 
Nitawafukuza wasivimalie vyeti vyangu
 
cheti kwanza mkuu
 
Wewe utoto wako kawashilikishe watoto wenzio tunawaza vitu vyenye tija unaleta mambo ya panya Hapa kwani umeambiwa hili jukwaa ni la wamakonde?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…