Ukimfumania mwenzi wako nyamaza

Ukimfumania mwenzi wako nyamaza

Ulimakafu

JF-Expert Member
Joined
Mar 18, 2011
Posts
31,248
Reaction score
13,244
Inashauriwa kuwa ukimfumania mwenzi wako-mke/mume, usipige kelele ili watu wasijue,maana watakucheka kuwa mpaka mwenzi wako kafika hatua hiyo wewe una dosari mahali au huwajibiki ipasavyo ndio maana kaamua kutoka.Kaa kimya kama kuachana iwe kimya kimya kulinda heshima yako.
 
Ushauri mwingine kama nguvu za giza
Kwanza niambie kama wewe una mwenza na kama unaye kweli hapa tunaweza kuongea
 
Acha kudanganya watu...heshima inatoka kwa aliyeshindwa kuanisha mapungufu yaliyopo ili yarekebishwe...aliyekosa staha na ujasiri wa kumwacha kabisa huyo “mwenye dosari“ za kudumu na kwenda moja kwa moja huko ambako anafurahia.

Hata siku moja mtu hatakiwi kuona aibu/kukosewa heshima kwasababu ya mapungufu ambayo pengine hakiyasababisha yeye au hata hayajui.Na mpenzi/mwenzi mzuri ni yule atakaefanya jitihada kukusaidia kuondokana na dosari zako badala ya kwenda kuonyesha kwa mwanaume mwingine kama unazo.Alafu unasema watu wanyamaze kutunza heshima wakati huko mwenzako anakoenda imeshashushwa mpaka sakafuni....?!
 
Inashauriwa kuwa ukimfumania mwenzi wako-mke/mume, usipige kelele ili watu wasijue,maana watakucheka kuwa mpaka mwenzi wako kafika hatua hiyo wewe una dosari mahali au huwajibiki ipasavyo ndio maana kaamua kutoka.Kaa kimya kama kuachana iwe kimya kimya kulinda heshima yako.

duuu
i hatari jaman....

NINASKIA UVIVU KUFIKIRI n so i thk tupo wengi WAVIVU WA KUFIKIRI.
 
Inashauriwa kuwa ukimfumania mwenzi wako-mke/mume, usipige kelele ili watu wasijue,maana watakucheka kuwa mpaka mwenzi wako kafika hatua hiyo wewe una dosari mahali au huwajibiki ipasavyo ndio maana kaamua kutoka.Kaa kimya kama kuachana iwe kimya kimya kulinda heshima yako.

Hii inanikumbusha ya jirani yangu ambaye alimfumania mkewe akimegwa na jirani yake. Alitoa maneno yoooooote ya ovyo ayajuaye. Akaamua kumrejesha mkewe nyumbani. Baada ya muda naona akatafakari uamuzi ule akaona hauna manufaa , akaamua kufanya mapatano na mkewe na sasa wapo pamoja. Kilichonisikitisha ni yale maneno ya ovyo aliyotoa juu ya mkewe na leo hii wapo pamoja tena.

Mie nakubaliana na ushauri wako wa kutulia na kuchukua maamuzi kimya kimya bila kutengeneza public scandal ambayo mwishowe inaweza kukutafuna wewe mwenyewe. Kumbuka: mpenzi wa kweli anauma na si rahisi kuachana naye kienyeji
 
Loh! ukae kimnya? nawajae mpaka wamwagike kama hakujiheshimu mwenyewe why mie nimuheshimu? atakua kajivunjia heshima yeye mwenyewe haihusiani na mimi,tena bora wajae ili akome na hapo hapo tumeshamaliziana,haijahusu kutoka nje ya ndoa nikwasababu mke/mume ana dosari ni tabia mbaya alonayo2 wala si kutokuwajibika.
 
Inashauriwa kuwa ukimfumania mwenzi wako-mke/mume, usipige kelele ili watu wasijue,maana watakucheka kuwa mpaka mwenzi wako kafika hatua hiyo wewe una dosari mahali au huwajibiki ipasavyo ndio maana kaamua kutoka.Kaa kimya kama kuachana iwe kimya kimya kulinda heshima yako.

Aliekushauri anaishi wapi? isije ikawa anaishi Dodoma....wewe una mke au mme?kama unae basi ana kazi..
 
Siwezi kunyamaza kamwe na wala sintapiga kelele kamwe,....atakaye nyamaza ama kupiga kelele ni yule aliyefumaniwa,......dawa ya mwizi mfukuze kimya kimya bana
 
Hayana formula haya,unaweza ukazimia definately mtu aliyezimia hapigi kelele
 
Kuna ukweli,haina faida yoyote kujaza watu na kufanya mambo ya kumdhalilisha kama kumpiga picha za utupu na mengineyo halafu kesho unaendelea kuishi nae nyumba moja.
 
Inashauriwa kuwa ukimfumania mwenzi wako-mke/mume, usipige kelele ili watu wasijue,maana watakucheka kuwa mpaka mwenzi wako kafika hatua hiyo wewe una dosari mahali au huwajibiki ipasavyo ndio maana kaamua kutoka.Kaa kimya kama kuachana iwe kimya kimya kulinda heshima yako.
Hivi kwenye kufumaniana kuna kulinda heshima????
 
Swala ni kutokwenda kichwa kichwa kama mbuzi aliyekatwa shingo,uwe umejipanga na maamuzi unayo tayari
nikiitwa leo nikamfumanie Mr siendi ili iweje baada ya hapo?

Back
Top Bottom