Tugepalu Jr
Member
- Oct 13, 2022
- 17
- 19
Katika maisha, tunakutana na Watu wapya wenye Tabia na sifa mbalimbali ambazo kwa namna moja ama nyingine huweza kuleta mabadiliko katika maisha yetu, aidha katika hali chanya au hali hasi.
Hivyo basi tunapaswa kuwa makini na wadadisi zaidi kabla ya kuamua ni yupi anaweza kuwa Rafiki kwako, yupi anaweza kukutunzia siri zako na yupi anaweza kuwa msaada kwako wakati wa kushuka kwako na kuinuka kwako, haijalishi ni wangapi wanamwona hata kama ni wewe peke yako lakini umempima na kuona kuwa anafaa katika wakati wako wa dhiki basi huyo ndiye Rafiki wa kweli.
Mshikilie kwa nguvu zako zote na kamwe usiuvunje moyo wake maana yeye alikuamini na akakukabidhi moyo wake bila ya kujali nini kitatokea wakati ujao, kafara aliyojitoa kwako iko na thamani kubwa sana kama utaamua kuithamini.
Tumekutana na marafiki wengi katika kipindi chetu cha ukuaji tangia tukiwa watoto wadogo mpaka kufikia ukubwani lakini wapo baadhi yao ambao hatuwakumbuki tena na tumekwisha wasahau kabisa, lakini pia wapo ambao hata litokee jambo gani au changamoto gani inakuwa ni ngumu sana kuwapoteza katika kumbukumbu zetu, hata kama hatujawaona kwa muda mrefu lakini wapo na wanaishi katika mioyo yetu daima.
Ukimpata Rafiki anayejua kuthamini uwepo wako katika maisha yake, hakikisha kuwa unamshikilia vyema na kuhakikisha kuwa huwezi kuuvunja moyo wake kwani Maumivu ya Usaliti ni Makali kuliko hata mtu aliyechomwa na mwiba.