Ukimsaidia ndugu yako usitegemee kurudishiwa fadhila/asante kutoka kwake

Ukimsaidia ndugu yako usitegemee kurudishiwa fadhila/asante kutoka kwake

Mkalukungone mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
862
Reaction score
1,755
Baadhi ya watu wamekuwa wakiwasaidia ndugu zao kwenye maeneo mbalimbali. Wengi wanaweza kuwasomesha, kuwapa kazi, kuwatibia pindi wanaumwa n,k.

Sasa baada ya kufanya hivyo wanaamini nao siku watarudishiwa fadhila au unaweza sema asante pale anapopata changamoto fulani. Sasa anapokosa msaada kutoka kwa huyo mtu aliwahi kumsaidia ananza kutengeneza chuki.

Acha nikwambie kitu wewe ukimsaidia mtu au ndugu yako wewe msaidie tu ili usiweke malengo kwamba na wewe siku atakusaidia, kwahiyo kama unamsaidia mtu ili na wewe kesho na keshokutwa aje akusaidie basi acha kabisa maana utaumiza moyo wako na kuingia kwenye mgogoro na huyo mtu.

Kama atatambua umuhimu wako mpaka yeye alipofika hapo basi yeye mwenyewe atakuja atakupa asante na kukusaidia kwa moyo wake wote.

Haya yangu ni hayo! Usiku uliokuwa mwema.
 
Back
Top Bottom