abdi basho
Member
- May 18, 2021
- 70
- 46
Ukosefu wa ajira umekuwa ni wimbo mkubwa ambao umeathiri asilimia kubwa ya vijana Afrika na dunia nzima kwa ujumla. Licha ya jitihada mbali mbali zinazochukuliwa kuwaajiri watu katika taaluma zao rasmi mfano ualimu, udaktari n.k. ni jambo la kawaida vijana hawa hawa wenye taaluma fulani kuwa na uwezo wa kufanya kitu kingine kwa mfano biashara, ukulima.
Nitajikita zaidi kwenye suala la ukosefu wa ajira na namna gani tunaweza kukabiliana nalo kupitia biashara na ujasiriamali, pia litahusu katika kupanua biashara kwa wafanya biashara wakubwa na wadogo, nitataja miongoni mwa nyenzo muhimu ambazo ni:-
1. Uaminifu: Vijana wawe waaminifu wanapopewa kazi, majukumu na vitu vya watu. Uaminifu ni kitu kimoja muhimu sana kwenye maisha. aminika
2. Hali ya kusaidiana: Watu wajenge sifa na hamasa ya kusaidiana ili kukamilisha malengo kama kundi, kijiji na taifa kwa ujumla
3. Ujuzi: Ni vyema kuangalia ujuzi wa mtu kabla hujampa jukumu lolote ili kuepusha lawama na kuharibu kazi. naamini ujuzi wa kujifunza au wa kuzaliwa.
4. Ufanisi: Unaweza kumfanyia mtu majaribio kuona je anafanya kazi zake kwa ufanisi wa kutosha n.k
Nitatolea mfano wa vijana wanaotumika kutangaza biashara mitandaoni hali ya kuwa biashara hawamiliki biashara hizo.
Kwa muda mrefu vijana wanaomaliza vyuo hujihusisha na biashara ndogo ndogo hasa zile matangazo mitandaoni(naweza kuita udalali) ambapo kijana yeye hamiliki duka lakini anapiga picha vitu kama vile nguo, viatu n.k. pamoja na biashara hizi kuwa na changamoto nyingi kwa mfano kutokuaminika kwa wateja kutokana na ongezeko la matapeli mitandaoni.
Kwa kiwango fulani biashara hii inakuwa ni ngumu kwa sababu ya kukosa uhalisia wa bei utakuta t-shirt ya elfu kumi na mbili(1,2000/-) yeye atataka auze kwa shilingi elfu ishirini(20,000/-) ili afidie mwenye duka apate faida na yeye apate faida zaidi mwisho wa siku kijana huyu anakosa wateja na kurudi kwenye wimbi la ukosefu wa ajira.
Kwa kiasi kikubwa vijana wameonekana kuziweza kazi hizi, tukimuamini kijana huyu na kumsaidia atafika mbali na atafikisha wengine mbali na mwisho wa siku tutajikuta kama taifa tumepiga hatua. cha kufanya muwezeshe kijana huyu kwa njia mbali mbali ikiwemo:-
1. Mpe bidhaa kwa bei ya jumla akauze kwa bei ya uhalisia hii itamuinua kijana huyu asiye na ajira na pia itakufanya na wewe uwe mfanya biashara mkubwa au kupanua soko la biashara yako sababu yeye atakuwa chanzo cha wewe kupata mauzo ya kila siku.
2. Kama ni biashara inayoweza kugawanyika fungua branch nyingine au muwezeshe afungue branch sehemu nyingine yenye mvuto wa kibiashara. kwa mfano wewe unauza mkaa kwa magunia upo kijijini unaweza kumbless kijana aliyepo mjini kwa gunia moja bure(ambalo ni sawa na faida yako ya siku moja) yeye atauza mjini kwa kuanza kupima kwa sado. atakua kibiashara wakati akikua yeye na wewe utakua kibiashara sababu atakuwa sasa wakati huo ananunua kutoka kwako na ataleta wengine na utapata wateja wengi sehemu tofauti tofauti.
3. Mpe ushauri wa jinsi gani anaweza kutumia nguvu zake na maarifa yake kupata mtaji.
Ili kuweza kumsaidia kijana huyu unaweza kuweka vitu vifuatavyo kwenye mazingatio, zingatia mambo yafuatayo:-
1. Utayari wa kijana, awe tayari kufanya kazi ambayo inawezekana si ktk taaluma yake lakini anaiweza vizuri.
2. Awe kijana muaminifu pia ukizingatia kama awe ndugu wa karibu n.k
3. Eneo analofanyia biashara zake, yaani liwe ni eneo la kibiashara kweli.
4. Uwezo wako, mpe support kadri ambavyo haitakuyumbisha.
HITIMISHO
Wenye biashara kubwa wajitahidi wawe wajasiriamali ili kuweza kutatua changamoto ya ajira nchini, unapo muinua kijana mmoja, umeinua mtaa, kijiji, wilaya, mkoa na taifa kwa ujumla. Pia vijana wachape kazi kwa uaminifu mkubwa na kujituma.

Upvote
2