Omutwale
JF-Expert Member
- Feb 4, 2008
- 1,429
- 1,047
Nimetooa methali hii kutoka lugha ya Kihaya. Wao husema: Olutega Mu-Kasho lwija na Nyoko
Na nimeikumbuka methali hii baada ya kutathmini nini kimetokea mpaka Babu, Shangazi, Wajomba na Bibi zangu kijijini wanaielewa vema hali ya ufisadi, siasa za maji taka, uwezo, udhaifu na mapungufu ya wagombea. Na kubwa zaidi wana-mwanga wa kutosha kungamua nini na kipi ahadi ya kweli na kama mtoaji anaaminika kuweza kuitekeleza. Baada ya kutathmini nimegundua suala la kufunga vyuo ili kukwepesha wanavyuo kushiriki kikamilifu katika kampeni na kuchagua viongozi katika maeneo walijiandikisha badala ya kuwa hasara limeguak mtaji lulu. Hawa wanafunzi walioshindwa kubaki mijini wanastaili pongezi baada ya October 31, 2010. Kiukweli binafsi nawapa heko maana utafiti wangu unaonyesha mchango wao kupanua mawazo huko walikokwenda umefanikiwa. Hapa ndiko Serikali ilimwekea mtego wa kifo mama wa kambo na sasa umerudi na maiti ya Mama aliyemzaa! Tuwashauri sasa wafanyeje!