UKIMWI na magonjwa mengine makubwa: Je, kipi hatari zaidi?

mhkk

JF-Expert Member
Joined
May 29, 2021
Posts
218
Reaction score
342
Kumekuwa na mijadala mingi kuhusu hatari za UKIMWI ikilinganishwa na magonjwa mengine makubwa kama figo kushindwa kufanya kazi, kansa, na kisukari. Watu wengine wanadai kuwa UKIMWI si hatari sana ikilinganishwa na magonjwa hayo. Ingawa ni kweli kwamba magonjwa kama figo, kansa, na kisukari yanaweza kuua kwa haraka, ni muhimu kuelewa kuwa UKIMWI hauzuia mtu kupata magonjwa hayo.

UKIMWI hudhoofisha kinga ya mwili, na hivyo kuongeza uwezekano wa mtu kupata magonjwa mengine makubwa, kama figo kushindwa kufanya kazi, kansa, au hata kisukari. Kwa mfano, mtu mwenye UKIMWI na ugonjwa wa figo yupo katika hatari kubwa zaidi ya kiafya kuliko mtu mwenye ugonjwa wa figo pekee. Hali ni sawa kwa kansa au kisukari; mwili ulioathiriwa na UKIMWI huwa na uwezo mdogo wa kupambana na magonjwa hayo.

Kwa hivyo, ni muhimu kuelewa kwamba UKIMWI sio tu ugonjwa pekee, bali pia hufungua milango kwa magonjwa mengine yanayoweza kuwa hatari zaidi. Ili kulinda afya zetu, tunapaswa kuepuka tabia hatarishi kama zinaa na kuhakikisha tunafanya maamuzi yanayolinda ustawi wa mwili na akili.
 
Umeuliza: Je, Kipi cha hatari zaidi?
Jawabu : Uzembe wa kutokuepuka tabia hatarishi kama zinaa na kuhakikisha tunafanya maamuzi yanayolinda ustawi wa mwili na akili.
 
Shida ya Ukimwi uko very preventive na kila siku yanaimbwa:
1.Usifanye ngono zembe
2.Tumia Kondomu
3.Usiwe na wapenzi wengi
4.Usi--share nyembe na vitu vyenye ncha kali
5.Mama mjamzito wahi hospitali, zalia hospitali ili mtoto awe salama.Usinyonyeshe
6.Usifanye ngono kinyume na maumbile
7.Pima na mwenza wako kabla n.k
Hapo ukipata watu wanakuhukumu - hata wewe unajihukumu kupita kawaida...
Hayo magonjwa mengine yanakuja tu - mengine genetics, n.k.

Maumivu ni yaleyale..Ukimwi unyanyapaa mwingi sana
 
Ukimwi ni baba wa magonjwa yote hayo.

Upungufu wa kinga mwilini unaleta magonjwa ya aina zote
 
Sema tu nyoosha maelezo ukimwi baada ya kuingia duniani ndio ulileta

Magonjwa haya yote yaani kifua kikuu, kisukari,presha, Figo , kansa, homa ya ini na mengine mengi

Ukimwi upita mlemle hayo magonjwa yote na Kaka na dada zake ukimwi

Tunajifichwa kwamba haya magonjwa ni tofauti lakini ukweli ndio huo
 
Ukimwi siyo ugonjwa (disease) bali ni hali ya mwili kukaribisha magonjwa (syndrome)
 
Back
Top Bottom