Mimi ni kijana muhitimu wa kidato cha nne, kiukweli tangu nipo shule, kubadili wasichana (playboy) ilikuwa tabia yangu, sikujali ki2, na kwa kuwa nilikuwa mzuri darasani wasichana hawakuacha kujipendekeza, na mimi sikufanya hiyana, niliwala kisawasawa, mwaka jana wakati tunasubiria majibu ya necta, nikapata tetesi kuwa kuna demu m1 ambaye nilitembea naye eti ameukwaa ukimwi,lol kwa kweli nlichanganyikiwa sana sikuwa na amani hata kidogo, mawazo ya kila siku yakanifanya nikonde, mafua mara kwa mara, viungo kuuma nikahic labda ni malaria, nikaenda kupima malaria ,nikakuta sina malaria basi ndo nikazidi kuchanganyikiwa, hakuna kitu nilichokiogopa kama kwenda kupima ukimwi kwa kuwa nilijua m nshaathirika tayari, kuna siku wazo la ujasiri likanijia, nikaona kwanini nateseka hivi huku sina uhakika, basi nilifikiria sana mbaka nikapata wazo la kwenda kupima japo kwa shingo upande ,nilipofika kituo cha afya nilitetemeka sana ilibaki kidogo nigeuze lakini nikapiga moyo konde nikaingia ndani , baada ya vipimo cha ajabu nikaonekana sina VVU, nilipata furaha ya ajabu isiyoelezeka, ila doctor akanishauri nirud baada ya miezi mitatu ,naapa ninapoongea miez mi3 imepita na nimetoka kupima tena majibu ni yale yale sina VVU, nina furaha ya ajabu, na nimeapa uplayboy nimekoma, jamani ukimwi usikieni kwa watu, 2 ..,pia nimejifunza jambo kuwa mawazo yanaweza yakaumba kitu wakati nahic nina vvu, mwili nao ukanipa support kwa homa za kwa mara lol, hofu inaua, JAMANI TUBADILIKE UKIMWI NI NOMA.