Ukimwi unaniuwa kwa haraka jamani

Joined
Mar 3, 2013
Posts
11
Reaction score
3
ninmwezi mmoja tu tambu ni fanye mapenzi na dada ambaye baada kumfanya tulienda maabara kupima maana nilimuona anavutia sana na alikuwa na umri wa miaka 19 tu hivyo nikaamini atakuwa mzima. Baada ya kumfaidi nikajenga hoja ya kujua afya zetu na tulivyopima sikuamini matokeo binti alikutwa na UKIMWI na hakuwa na wasiwasi kabisa akaanza kunipa pole.

Naomba msaada wandugu kama kunaaina ya kipimo ambacho naweza kufanya nikawa na uhakika wa afya yangu maana mala tumbo, kichwa, usingizi saa 8 unakatika, kichefuchefu, mafua na kikohozi, mwili kuwasha. hayo ni machache tu kwa dalili na magonjwa niliyonayo.

haja yangu sio kujianika kwa umalaya wangu bali nimeamua kuandika hapa nikijieleza kwa DR ili niweze kupata msaada wa aina ya kipimo maana rapid test inaonyesha hakuna tatizo lakini mpaka miezi mitatu ndipo huwa na uhakika lakini iwapo kunakipimo ambacho naweza kujua hali yangu ndani ya hizi wiki 6 tangu nikutane kimwili na yule dada nitafurahi.
 
tumia tafsida..kama kujamiana, kugegedana, kufanya mapenz hata kukutanisha vkojoleo
 
Yaani mwezi mmoja tu uanze kupata magonjwa nyemelezi?!!.
Wewe utakua umepanick.
 
Tulia mkuu!!sio lazima uathirike kwa kufanya ngono na mwathirika,by the way hujatueleza kama ulipiga kavukavu au la,let's take it kavukavu,you still have a chance to survive,subiri uathirike,usijiathiri mwenyewe kwa mawazo,siamini kwamba kweli umekosa sehemu ya kupima hadi uje jf kupimwa kwa keyboard,nenda kwanza hospital kapime then uje hapa kutafuta ushauri,ila pia uwe tayari kukutana na ma bush counselors watakaokupa ushauri wa aina ya Fasouls .pole sana baba nanii.
 
Last edited by a moderator:
Ukienda hospitali waambie wakufanyie elisa test. Hii inaweza kutambua maambukizi hadi ya masaa 32. Magomeni kuna hospitali wana hicho kipimo, sina uhakika wapi. Agha khan nadhani watakuwa nacho.

hivi zile dawa za kuzuia maambukizi kwa mtu aliyekutana na dam yenye maambukizi hufanya kazi kwa watu walio zini??
 
Pole sana ndugu yangu yangu kwa hilo,ila mimi nina mambo kadhaa ya kuksema:

Kwanza sio kila unapofanya mapenzi na mtu mwenye VVU utaambukizwa. Kumbuka tumekuwa tunafanya mambo haya mara kadhaa na watu wenye VVU bila kujua na hakuna shida yoyote tunayopata;ni bahati nzuri tu kwamba nyie mlienda kupima soon after hilo tendo..huo ni ujasiri wa hali ya juu na unastahili kupongezwa.

Pili,huna haja ya kukosa amani kiasi hicho.Hilo limeishatokea,limetokea,unachotakiwa ni kufocus mbele na kuendelea na maisha yako kama awali.Najua hii ni chungu kumeza,lakini je ikiwa umeambukizwa,what next?! Hakuna haja ya kuhangaika mahospitalini kutafuta kipimo,unaweza kukipata kwa gharama ya juu sana,maana inaonekana uko radhi kutoa kiasi chochote cha pesa mradi tu ujue afya yako.Swali,sasa ukishajua umeambukizwa,nini kinafuata?! Na je ukiambiwa hujaambukizwa,unadhani itakuwa kinga ya kuzuia kuambukizwa tena?! Nachotaka kusema hapa ni kwamba wewe endelea na maisha yako kama kawaida huku ukisubiri hiyo miezi 3 ipite ukapime tena ili kujiridhisha..

Inavyooneka wewe ni kijana na yumkini upo chuoni,unachotakiwa kujua ni kwamba bado unayo safari ndefu ya kuishi.Utakumbana na mengi tena mazito kuliko hili,jaribu kuwa mstahimilivu.Hili limetokea hivi leo,hujui mwaka kesho utakuja hapa na lipi,so kwa muda huu wewe concetrate with what you're doing.Usije ukapoteza hata unachokifanya,halafu mwisho wa siku unapima unakutwa uko salama..
 
Ukienda hospitali waambie wakufanyie elisa test. Hii inaweza kutambua maambukizi hadi ya masaa 32. Magomeni kuna hospitali wana hicho kipimo, sina uhakika wapi. Agha khan nadhani watakuwa nacho.

aspate tabu aende muhimbili kwenye blood donors unit ajiseme anatoa damu kwa kujitolea so wao wana uwezo wa kupima hata 24 hrs baada ya maambukizi kama hajiamini. na majibu kwao ni siku ya j4 na alhamisi tu saa 2-6 mchana
 
hivi zile dawa za kuzuia maambukizi kwa mtu aliyekutana na dam yenye maambukizi hufanya kazi kwa watu walio zini??

Inaweza kufanya kazi vizuri tu,but we are not entertain it!! Unsafe sex at your own risk.
 
Inaweza kufanya kazi vizuri tu,but we are not entertain it!! Unsafe sex at your own risk.

ahaaaaaaaaaa mie nlikuwa sijui hiyo nilizoea kuona zinatumika kwa hasa watu wa maabara tu
 
ahaaaaaaaaaa mie nlikuwa sijui hiyo nilizoea kuona zinatumika kwa hasa watu wa maabara tu
Be carefull Dadaa,tunataka kuweka mazingira ya kutoathirika,na siyo kuathirika na ku process consequence,jichunge.
Naona umecheka kweeeeeeli,usidhani umepata tiba mbadala,tatizo bado liko palepale.
 
Be carefull Dadaa,tunataka kuweka mazingira ya kutoathirika,na siyo kuathirika na ku process consequence,jichunge.

asante kaka kwa ushauri wako, but usiwe na hofu juu yangu kabisa.
 
Be carefull Dadaa,tunataka kuweka mazingira ya kutoathirika,na siyo kuathirika na ku process consequence,jichunge.
Naona umecheka kweeeeeeli,usidhani umepata tiba mbadala,tatizo bado liko palepale.
hahahhahaha! kaka sicheki kwamba nimepata tiba mbadala na nafkiri kwamba hujanijua vyema ila ungekuwa unanijua basi ungejua kwanini nimecheka.

binafsi na deal na vijidudu vya magonjwa katika tafiti so hawa wadudu nacheza nao kila siku asbh mpaka jion mwaka mzima as MBO'S
 

MBO's maana yake nini?
 
My brother Mwakambaya2013
kama ni muumini na una amini katika Mungu, mludie na ukili kuto kurudia mfumo wa dhambi, ukichukua hatua hii itakusaidia kaka, uwezo wetu ufikapo mwisho hatuna budi kujikabidhi kwa Mungu, kwani utakua mwenye amani ndani ya nafsi yako itayo kujenga.
Hapa jamvini si kila mtu ana roho ya imani au mwenye kuguswa na matatizo ya wenzake..

Daima mtegemee Mungu na usihofu wala kukata tamaa Mungu anakupenda
 
Last edited by a moderator:
Elisa ni kipimo cha uhakika ila unaweza ukajijuapia.

Kama baada ya ngono ulipata homa kama ya flu, au mwili ukawa kama una surua vile, uwezekano kama umepata maambukizi ni mkubwa.

lakini wewe, watu wanaimba nyimbo, michezo ya kuigiza, filamu matangazo kila aina, documentaries zote unaona ni bure?
Huna huruma kabisa kwa watu wanaokupenda.
Sikunyanyapai lakini hustahili moral support kwani haionyeshi kama ni bahati mbaya bali ulifanya makusudi ukijua fika hatari ya ngono zembe.
Hata hivyo I hope uko salama, nisingependa mtu yeyote apate maambukizi. I have been affected so many times by AIDS in the FAMILY
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…