x - mas
JF-Expert Member
- Oct 5, 2012
- 931
- 612
Habari za masiku wana jf wapendwa wangu.Baada ya miangaiko mingi na majaribio ya miradi mbalimbali hatimaye nimebahatisha kamradi, kiasi fulani kana faida kamradi kenyewe ni cha kutoa huduma ya usafirishaji wa mizigo na abiria kwa kutumia guta(pikipiki ya mataili matatu)huku kijijini ni dili kwani usafiri ni washida. Nimekuwa nikiandika kumbukumbu za biashara yangu tangu siku ya kwanza nilipo ianza hyo biashara.Kumbukumbu hzo ni kama gharama za petrol,vipuri,matumizi ya mahtaji yangu muhmu pamoja na faida ninayo ipata kwa siku. Baada ya miaezi kadhaa tangu nianze kabiashara changu nilikaa chni na ku tathmin mradi wangu hivyo ili nipasa nichukue daftari ya kumbukumbu,nikatafuta jumla ya kipato changu kwa miezi hyo kisha nikatoa ghalama za petrol,vipuri matumizi yangu ya lazima ya kilasiku kiasi kilichobaki ndio faida yangu kweli faida ilikuwa kubwa sana lakini......inaendelea,