Ukimya wa wapenda Nchi

Ukimya wa wapenda Nchi

FATHER OF REALITY

Senior Member
Joined
Nov 3, 2014
Posts
123
Reaction score
100
Bila Shaka sasa Nchi inaenda vizuri katika mwendo ambao tunauhitaji na tumeridhika nao, ishara ya hili inajionesha pale wakosoaji na wapenda nchi, yaani wazalendo nguli waliojitokeza kipindi cha hayati JPM kunyamaa Kwa kimya kikubwa.

Nadhani sasa mambo yapo safiiii, kijamii, kiuchumi, kiutamaduni na hata kisiasa, ndo mama Kigogo kanyamaa, mpenda nchi huyu, na na wengine wengi.

Sasa kiuchumi hata kama nchi inakopa, tunaona pesa iendako.
Ukichunguza vizuri kutokana na ustawi huu utagundua kwamba wakosoaji wa serikali ya awamu ya tano ya JPM walikuwa ni wazalendo hasa, na watetezi wa wanyonge, na Kwa sasa imewapasa kunyamaa maana mambo ni shwari mno.

Hakuna mifumuko ya bei, na hata kama ipo ina sababu yakinifu, ajali zimetoweka Kwa Kasi, ujambazi, hamna tena, na swala kuuawa maalbino limebaki historia, ukandamizaji wa kisiasa hakuna tena, dawa za kulevya tunapambana nazo, serikali inakopa kwa mpango maalum si kama hapa ktkt awamu ya JPM, nidhamu maofisini imekuwa ni ile ya kweli si ya uwoga, umeme haukatikikatiki na ikiwa hvo tunaelezwa sababu za maana, mama ntilie, machinga, bodada n.k wanatafuta mkate wao Kwa Uhuru.

Nafurahishwa na wazalendo wa nchi hii, kwanza namna wafanyavyo harakati zao, harakati huja muda muafaka hasa tunapokuwa shidani. Si kama sasa, ambapo kuna shida zenye maelezo kuntu, ambazo kimsingi si shida, uhaba wa maji mfano, umechangiwa na unywaji wa kiwango kikubwa wa wanyama wafugwao, umeme ukame, tozo, maendeleo, kuapanda umeme kufidia gharama za uendeshaji, mafuta Vita vya Urusi na Ukraine. Ruzuku ya mafuta bil 100 imetolewa ili kulegeza bei kidogo, na tumeona bei imepoa.

HIVI TULIIMBA WIMBO WETU AU TULIIMBISHWA WIMBO WAO?
 
Nchi inaenda vizuri kama unachukia umeme kukatika kila mara hamia chato

Km unachukia wamasai kutimuliwa kwenye ardhi yao ya asili na kupewa waarabu jinyonge ti
 
NA KWA SBB HIZI, MAMA APEWE MPAKA 2040. AU VIPI PRAISE TEAM?
 
Bila Shaka sasa Nchi inaenda vizuri katika mwendo ambao tunauhitaji na tumeridhika nao, ishara ya hili inajionesha pale wakosoaji na wapenda nch...
Mkuu wakati huu ni WA kunywa mvinyo tu kelele na ukosoaji sio wakati wake tulichokitaka tumekipata sasa kelele za nini tena
 
Unamuongelea mtu mmoja tu hapa!
 
Back
Top Bottom