Ukimya Wetu Watanzania ndio unaotuponza katika suala la Tozo na Katiba Mpya

Usikimbie hoja. Hoja hapa ni nini hasa maana ya "maendeleo". Wewe umeeleza maendeleo kama ni ujenzi wa miundombinu. Sasa hapo juu ndio umefafanua zaidi. Hoja yangu ni kwamba uhuru wa watu ni muhimu zaidi. Watu ndio waamue wanataka nini hasa.
Tanzania hakuna Uhuru wa kutoa maoni. Kuna magazeti mengi yamefutwa kabisa, mengine yamefungiwa. Kisa? Yalisema UKWELI ambao hauifurahishi serikali.

Tanzania pia kuna ubaguzi mkubwa sana. Raia daraja la kwanza ni wale wanaoshabikia ccm na serikali yake. Raia daraja la TANO ni wale wanaoshabikia UPINZANI. Na ukumbuke, hii ni nchi ya Demokrasia ya Vyama Vingi, kwa mujibu wa katiba, Sheria na Kanuni. Lakini bado, kwa UDHAIFU wa Katiba yetu, hawa wa daraja la TANO wanaweza kuteswa, kunyanyaswa, kupotezwa, kuuwawa, kirahisi tu na hakuna anayetaharuki au kushangaa.
Nimesema habari ya Magazeti kufungiwa. Kuna gazeti la Uhuru karibuni limefanya kosa kubwa sana. Limeandika habari ya uchochezi dhidi ya Rais. Angalia adhabu yao: kufungiwa wiki mbili!

Tunachotaka hii ni nchi yetu sote. Wote ni watanzania. Kukiwa na uhuru wa maoni, Magazeti yafumue uozo. Yakikosea si mahakama zipo? Serikali ifungue shauri. Bunge liwe kweli Bunge la vyama vingi. Sio wapinzani wanahujumiwa kihunihuni tu, na mambo yanakwenda.

Msikilize Bashiru Ali kuhusu Katiba Mpya:
Your browser is not able to display this video.
 
Nenda mtaani kulianzisha sasa ukikaa humu unaishia kuwa mjinga na kujichosha bure maana humu kila mpinzani huwa anaongoza kura ila kwenye uchaguzi anaangukia pua.
 
Serikali iache matumizi ya anasa

MaV8 na Maposho

Sekta binafsi umedorora

Wananchi hawana Pesa, umasikini umeongezeka

Serikali ibane matumizi
 
Mila na desturi ya kiTanzania tunasema mwenye nguvu mpishe. Kwisha

Uanze kupambana na serikali utaweza wewe? Kukifumuka machafuko watoto unawapeleka wapi
 
Hawa huvuna bila kupanda walianza kupiga pesa za raia tangu zama za wastaafu wa EAC, wazee hao wakaambulia kuchekwa na awamu zote.

Kisha wakubwa wakatinga kwenye akiba za wafanyakazi za PPF, NSSF nk. Wamenogewa na kuleweshwa kwa utamu wa pesa ya dhuluma.

Sasa wamebuni shamba la bibi jipyaa! Linaitwa TOZO. Kwa kicheko wanaendelea kuvuna bila kupanda!
Tukilia wanasema tunapiga kelele kwa kufurahia maumivu!

Wanasahau kwamba huu ni mchezo wa nyoka kutaka aishi kwa kula mkia wake!

Tulisema enzi za JPM tukaonekana adui wa maendeleo, kama ilivyo tozo sasa. Kisingizio ni maendeleo!

Nyerere aliongelea mambo ya kuzoea kula nyama ya mtu. Ilikuwa parable tu. Ukila pesa ya dhuluma hutaacha, utazoea.

Sent from my G80 using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…