Ukinunua gari kwa dalali, wasiwasi

Ukinunua gari kwa dalali, wasiwasi

Joined
Aug 5, 2022
Posts
88
Reaction score
119
Najua ujanja duniani ni mwingi Sana.

Gari la mkononi ni chombo ambacho usipokuwa makini unapigwa mchana kweupe pee.

Wengine Hadi wanaacha kuagiza Japan au uarabuni ni hofu ya kupigwa.

Mimi ni miongoni mwao. Madam hakuna kampuni nchini itayonohakikishia gari chessis namba flani IPO na mmliki Halali ni Mr x nabaki kuangalia alternatives.

Narudia sipendi kupigwa...nimeish maisha yangu kama ni kupigwa inatoshasana.

Nakumbuka tangu enzi unaambiwa na vibaka mdudu?! Kumbe wanakupiga.

Nimeamua nichukue chima Kwa MTU,

JF ni shule kuu nAelewa.. nilipata kuambiwa hapa uende na namba ya gari ukaichunguze kama sio ya wizi. Lakini bado nipo kwenye Lindi la maswali.

Je nipewe KADI ya gari najua.
Je nikipewa KADI feki? Nipeni maujuzi. Dalali akiuza humuon Tena.

Na je usajili kubadili Jina la umiliki ikibuma?? Makandokando gani yaweza tokea??

Bado ninamaswali mengi.

JF ni shule kuu Msaada wa tahadhari.

Nikinunua gari via dalali wasiwasi hauniishi
 
Ukipewa kadi verify TRA unaweza kwend hata kwenye ofisi zao...

Angalia madeni ya gari TRA, Police, check Bima.

Ita fundi unayemuamini akague gari na usikubali fundi azoeane na dalali au mwenye gari atakuzunguka. Ikiwezekana asijue kama unanunua wewe...

Usiuziwe gari kwenye picha....

Pamoja na gari sio body ila kagua rangi ipasavyo na angalia kama ishawahi kupata ajali. Mafundi wengi wanajua...

Mwisho.

Gari gani unataka kununua?
 
Jamaa unaandika kama unaongea, yani unamsimulia mtu anae ijua stori yako.

Andika kama msomi tukuelewe, tukusaidie, na utusaidie.

Aliye elewa alicho andika mpasha habari, anieleweshe.
 
Back
Top Bottom