BigTall
JF-Expert Member
- Mar 9, 2022
- 525
- 1,257
Huduma hii ni salama akiipata kwenye kituo cha afya kwani ataweza kupata huduma ya kusafishwa kizazi , atapata ushauri wa kisaikolojia, elimu ya uzazi wa mpango, ataweza kuongezwa maji au damu endapo atapungukiwa, atafanyiwa uchunguzi wa saratani ya Mlango wa Kizazi na Saratani ya Matiti, atachunguzwa magonjwa ya ngono na ya kuambukiza.
Msichana na mwanamke katika kuokoa Maisha yako unapoona dalili za mimba kuharibika nenda kituo cha afya kilicho karibu na wewe usipate huduma ya kienyeji.
#Afyayauzazi #Afyakwanza #Afyakwawote
***********
Huduma ambayo mwanamke anatakiwa kuipata kitaalamu inaitwa Comprehensive Post Abortion - (cPAC) ambayo kwa Kiswahili inatambulika kama “Huduma Baada ya Mimba Kuharibika”, hii hutolewa kwa ajili ya kulinda usalama wa afya ya mwathirika wa tukio, wataalamu wa afya wanasema huduma huu ni muhimu sana kwa mwathirika.
Baadhi ya huduma za cPAC ambazo mwanamke anatakiwa kuzipata ndani ya muda mfupi tangu kuharibika kwa mimba au kutolewa ni:
-Kusafishwa kizazi (usafi wa kizazi), kupewa ushauri wa kisaikolojia, kupewa elimu ya afya ya uzazi
-Kukupewa dawa maalum, kupewa au kuongezewa maji, damu n.k
-Kuchunguzwa Saratani ya Matiti
-Kuchunguzwa magonjwa wa zinaa kama vile H.I.V au gono
-Kuchunguzwa magonjwa ya kuambukiza
-Kupewa ushauri wa afya ya kizazi na saikolojia
-Huduma ya kuchunguzwa Saratani ya Shingo ya Kizazi
Pia soma > Mbunge azungumzia Utoaji Mimba usio salama kuwa unazidi kuendelea Nchini Tanzania