Mjengwa siku hizi anajifanya Masiha
Maggid Mjengwa Nimepiga kura Nyalumbu, Kilolo, Iringa. Niliongozana na wana wangu. Hali ilikuwa ni ya utulivu mkubwa. Kituo changu kilikuwa na waliojiandikisha 394. Kubwa kabisa lililonigusa ni pale Mama mtu mzima aliyehitaji msaada wangu ili aweze kupiga kura. Hakujua kusoma na kuandika. Aliulizwa kama anahitaji msaada wa mtu anayemwamini. Alinigeukia, akaniambia; " Mwanangu njoo unisaidie". Alikuwa akiangalia picha na rangi. Kazi yangu ikawa kumsomea na kumtilia tiki. Sitasahau, na naliona jukumu lililo mbele yetu.