Ukiona mwenzako ananyolewa. Kwa mara ya kwanza siku ya jana umeme umekatika usiku mzima katika mtaa tunaokatiwa mara chache

G Tank

JF-Expert Member
Joined
Feb 9, 2023
Posts
2,297
Reaction score
8,760
Huu mtaa tulishani hatuguswi na matatizo ya umeme kukatika usiku, siku ya jana umeme umekatika mida ya saa tatu tukadhani utarudi saa nne, subiri mpaka tano hakuna kitu.

Ni mpaka asubuhi saa mbili ndio umewashwa, hapa watu wameanza kuchaji power bank zao na kunyoosha nguo jioni muda huu.

Nadhani jana ilikuwa ni ukaribisho wa mgao unaoweza kudumu kwa muda mrefu sana.
 
Poleni na diesel, petrol, kerosene inapanda bei soon
 
Huu mtaa tulishani hatuguswi na matatizo ya umeme kukatika usiku, siku ya jana umeme umekatika mida ya saa tatu tukadhani utarudi saa nne, subiri mpaka tano hakuna kitu.

Ni mpaka asubuhi saa mbili ndio umewashwa, hapa watu wameanza kuchaji power bank zao na kunyoosha nguo jioni muda huu.

Nadhani jana ilikuwa ni ukaribisho wa mgao unaoweza kudumu kwa muda mrefu sana.

Huu ndo muda muafaka sasa wa kununua solar panels..

Au chanzo kingine cha nishati ya umeme.
 
Back
Top Bottom