Ukiona una hela halafu haujui ufanyie nini, hiyo Pesa kupotea ni rahisi sana.

Ukiona una hela halafu haujui ufanyie nini, hiyo Pesa kupotea ni rahisi sana.

Jumanne Mwita

JF-Expert Member
Joined
Nov 18, 2014
Posts
530
Reaction score
1,446
Katika biashara ni muhimu kufanya kitu ambacho unakiridhia kutoka ndani ya moyo wako, ili ukikutana na changamoto usitupie watu lawama.

Mtu mwenyewe ndiyo uamue kipi upo tayari kukifanya halafu kuanzia hapo ndipo tuanze kupeana muongozo hii biashara vipi bhana ikoje?

Biashara siyo IDEA TU, Kuna mengi katika biashara.


Kabla ya kuomba ushauri njoo na wazo lako ninafikilia kufanya biashara hii unaonaje? Kama unafahamu mwambie ukweli hasara na faida achanganye mwenyewe afanye au aache. Sikuzote mawazo mengi huwa ni mazuri tu hakunaga mawazo ya kukandia na onyo haipo, mengi huwa ni faida tu.

Pia endelea kumuuliza aliye kuletea mada hiyo kwamba! wewe unafikiria nini..kama unaona hana chochote anacho fikiria basi mwambie tu ukweli tulia kwanza kama kuna sehemu pa kuiweka kaiweke kwanza..ukipata chochote nitafute..

kwasababu utampa ushari labda "matunda yanalipa na utampa faida na utokaji wake kiujumla kwa kawaida huwa tunapeana faida tu..nikakupanga ukanielewa ukaanza, kipindi unaanza ukaona faida ila kila unaponunua mzigo unakutana na matunda mengine yameharibika zaidi ya trip zote" Unazonunua.

Hapa ndo tunarudi kulaumiana kwamba mwana kanipoteza kumbe biashara yenyewe hasara tu kila nikinunua mzigo. Anasahau hakuna biashara inayolenga faida tu ila kwa sababu wewe ndio umemshauri akatia nguvu yake. Jiandae kwa lawama.
 
Back
Top Bottom