Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Bonjour !great thinkers hivi naomba kuuliza je ukiugua na umepata upungufu wa damu je? Dna itabadilika ? Au hiyo damu huwa inajitenga ?na kama inajitenga inaenda wapi? Jamani mwenye jibu naomba anipatie
Jee ina maana sample ya damu si vema kuitumia kupata DNA profile ya mtu, na hasa kama amewahi kuongezawa damu?
Nakubaliana 100% na wachangiaji Riwa na paulss kuongezewa damu ni kwa ajilil ya kuweza kuboresha usafirishaji wa hewa safi (oygen) kwenda sehemu mbali mbali za mwili. Mtu ambaye anaongezewa damu anapewa chembe chembe nyekundu (red blood cells) ili kumsaidia kwa muda mfupi wakati mwili wake upo kwenye mchakato wa kufidia upungufu uliopo. Kwa maana hiyio hizo chembe zinakuja na DNA yake na hazina uwezo wa kubadilisha DNA ya mpokeaji wa damu.
Sasa DNA kwenye Damu inatofautishwaje iwapo damu ndo itatumika?
Mkuu mleta mada umeuliza swali moja zuri sana..
JIBU LA SWALI LAKO NI "HAPANA" au kwa kirefu naweza sema "HAKUNA NAMNA ya DNA(Vinasaba) kubadilika"
Damu huwa imeundwa na vitu vinne;
1. Red blood cells-RBC (Chembe Hai Nyekundu)
2. White blood cells-WBC (Chembe Hai Nyeupe)
3. Platelets
4. Plasma.
Sasa ni ukweli uliopo ni kuwa WBC (Chembe Hai Nyeupe) ndio huwa inabeba DNA (Vinasaba) na kawaida lengo kubwa la "Blood transfusion" ni kuongeza Chembe Hai Nyekundu ambazo kiasili huwa hazina Vinasaba.
Wakati pekee ambapo unaweza ukahamisha DNA ya mtu mmoja kwenda kwa mtu mwingine nayo ni rarely sana, ni pale mtu anapoongezewa Bone marrow "uboho".
ok umesema kwenye damu kuna vitu vinne na kinachobeba DNA ni WBc.swali je wakati mtu anongezewa damu Hiyo WBC inatolewa kwenye damu? Na kama haitolewi je mtu akisha ongezewea damu sasa si atakuwa na DNA zake pamoja na huyo aliye muongezea damu? Ufafanuzi tafadhari na hata kama zipo kidogo je hazionekani?na kama zinaonekana zinakwenda wapi? Au ina baki mchanganyiko wa DNA au mpaka wazungu waje watujibie au kuna baadhi ya watu walikwisha pewa majibu feki ya dna kutokana na kuwa waliongezewaga damu? Au kwa vile hatuna wataalam kwa hiyo jibu lolote ni sawa.nitarudi baadae.