Ukipata kipya usisahau cha zamani

Ukipata kipya usisahau cha zamani

Kisai

JF-Expert Member
Joined
Apr 6, 2018
Posts
28,481
Reaction score
28,749
Nawakumbusha wanaume wenzangu wote wenye mke zaidi ya mmoja. Mke mdogo asikufanye ukamsahau au ukampuuza mke mkubwa.

Mke mdogo amenifanya nizidi kumpenda sana mke mkubwa.

Naongea kikubwa kwa elimu na maarifa na kwa insafu tuwapende wake zetu, watoto zetu na wale walio karibu yetu.

Ukweli ulivyo ni kuwa mbora wetu kwa sisi wanaume ni yule ambaye ni mbora kwa wake zake, watoto wake.

Asanteni sana.
 
Nachojua Upendo haugawanyiki
Kijana naona siku hizi umekuwa unaandika mambi ya uongo sana.

Upendo unagawanyika endapo ukijua wewe ni mwanaume na wajibu wako ni nini.

Wanaume tumeumbwa kumiliki mke zaidi ya mmoja ndiyo maana hili kwetu ni jambo sahali sana.

Kisichowezekana ni kuwapenda wake zako wote kwa upendo ulio sawa (hapa tayari umeshagawanya upendo),sababu mapenzi na upendo huchagizwa na unaye mpenda. Ila kinachowezekana ni wote kuwahudumia kwa stahiki zao.

Hata kwa watoto,kwa sisi tulio ruzukiwa watoto,huwezi kuwapenda watoto wako wote sawa ila tunaweza kuwahudumia wote kwa usawa.
 
Ndio maana nimesema kwamba Upendo haugawanyiki. Kuna utakae mpenda zaidi iwe kwa watoto au mke. Ndio mfumo wa maisha unless otherwise Unataka ligi tu mkuu
 
Hapo tayari ushaugawanya huo upendo,ndiyo maana yule unampenda kidogo yule unampenda sana.
Kwakua upendo haugawanyiki basi inabidi uoe yule tu unayempenda ambae huwezi shea upendo wake na wengine.
 
Back
Top Bottom