Ukipata muda, sikiliza Interview ya Mgunda dhidi ya De Agosto

Peramiho yetu

JF-Expert Member
Joined
May 25, 2018
Posts
5,303
Reaction score
14,983
Mara baada ya mechi kocha alihojiwa juu ya ushindi ule hapa DSM dhidi ya Primiero De Agosto.

Mtangazaji: Vipi matokeo ya leo unayaelezea vipi?

Mgunda: Nawashukuru wachezaji wakongwe kikosini wakiongozwa na Kapt. John Boko, Erasto nyoni, Jonas Mkude na Chama kwa kunisaidia kunipa mbinu.

Kama kocha alijishusha mno na kusahau mbinu zake na akaamini mbinu za wakongwe kikosini.

Na jana akaona isiwe tabu akaona awaanzishe wakali wa mbinu ili amalize mchezo.

Kilichotokea mmekiona.

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
Kwani kuna team gani duniani ambayo haifungwi mashabiki wa bongo kweli hatujielewi
 
Kwani kuna team gani duniani ambayo haifungwi mashabiki wa bongo kweli hatujielewi
Kwann sasa Yanga akifungwaga huwa mnashoboka kama unalijua hili La timu zote kufungwa duniani
 
Ndugub kuna wanasimba hawataki kuambiwa ukweli Kuna group Moja niliwaambia ukweli leo kuwa bocco,,nyoni,,matola muda wao umekwsha wakanijibu na wadharau wachezaji na kuwakashfu...... lastly wamen-remove kwny group
 
Kwann sasa Yanga akifungwaga huwa mnashoboka kama unalijua hili La timu zote kufungwa duniani
Yanga si kaadhimisha unbeaten juzi kafungwa lini yanga?
 
Ndugub kuna wanasimba hawataki kuambiwa ukweli Kuna group Moja niliwaambia ukweli leo kuwa bocco,,nyoni,,matola muda wao umekwsha wakanijibu na wadharau wachezaji na kuwakashfu...... lastly wamen-remove kwny group
Ongezea na Jonas mkude.

Najua huyu wengi wanampenda, ila kwa miaka ya karibuni katikati akicheza mkude au Mzamiru basi timu inakosa utawala wa eneo la katikati na ubunifu wa kwenda mbele.

Simba haina namba 6 na namba 8 wakuleta matokeo mechi ngumu.
 
Hata mimi nimeshangaa tena wakataja kwa majina kabisa watu fulani ndio wamemsaidia .
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…