UKipewa masaa 6 kukata mti, tumia masaa 4 kunoa shoka

Dr Jeremiahs

Member
Joined
Sep 4, 2020
Posts
39
Reaction score
306
Rais wa 16 wa Marekani, Abraham Lincoln aliwahi kusema “Ukipewa Masaa sita ya kukata mti, tumia masaa manne kunoa shoka” kwa maneno mengine ni kuwa utatumia nguvu nyingi sana kuangusha mti ikiwa shoka lako litakuwa butu.

ALIKUWA NA MAANA GANI? Alimaanisha kwamba Ukitaka kufanikiwa kwenye mambo yako kwa ufanisi basi usifanye mambo yako kwa kutumia nguvu nyingi bali tumia akili, Fanya maandalizi ya kutosha kabla ya kuingia kwenye jambo lako. Ukitumia nguvu sana kwenye mambo yako basi kuna uwezekano mkubwa wa kutokufanikiwa.

Dunia haiongozwi na watu wenye nguvu nyingi au wenye pesa nyingi, Dunia inaongozwa na watu wenye akili, Smart minded people. Na si wote walizaliwa wakiwa na akili nyingi (Genetically Genius) kuna wengine walipata akili baada ya kutafuta hekima, ujuzi na maarifa kutoka kwa wengine kupitia mentorship na kwa kusoma sana vitabu.

Kama wewe ni miongoni mwa waliokosa matumizi ya logarithm kwenye maisha ya kila siku, basi utakubaliana na mimi kuwa miaka mingi tuliyotumia kusoma shule tulijifunza vitu vingi sana ambavyo havina matumizi ya moja kwa moja katika maisha. Jambo amblo limepelekea kuona BIASHARA kama mkombozi aliyebaki kutuepusha na fedhedha itokayo na kuwategemea wengine kiuchumi.

Ndg, kosa la kupewa SHULE ambayo mpaka sasa haijakusaidia halikuwa la kwako, lakin kufanya BIASHARA bila kuwa na Elimu sahihi ya biashara ni Shimo unalojichimbia mwenyewe. Ikiwa uliweza kutumia Zaidi ya miaka 20 kusoma vitu ambavyo hajakusaidia kwanini basi usitume walau miezi sita kuisoma vizuri biashara unayotaka kuifanya.

Katika ulimwengu huu wa utandawazi mambo yamerahisishwa sana, leo hii mtu anaweza pata Degree ya Sheria kutoka vyuo mashuhuri bila hata kuingia darasani. Hivyo basi usitumie muda wako kusoma habari za watu kwenye mitandao ya jamii, bali tumia mitandao hiyo kama FURSA.

Keep Winning
I am Smatt
 
Andiko bora sana limenibless asubuhi hii ya leo, natoa shukuran zangu za dhat halafu nakufollow.
 
Back
Top Bottom