Ukipinga vifungu vya mkataba chawa wanakwambia haujasoma mkataba, umemsikiliza Prof. Shivji na Prof. Tibaijuka

Ukipinga vifungu vya mkataba chawa wanakwambia haujasoma mkataba, umemsikiliza Prof. Shivji na Prof. Tibaijuka

Mwande na Mndewa

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2021
Posts
1,117
Reaction score
3,153
Niwaambie chawa, kwenye Chuo Kikuu chochote Senior intellectual akiongea wengineo tunasikiliza, sasa chawa wanatujazia propaganda na wamejipanga na majibu yao, ukiwaambia mkataba unazungumzia bandari zote za Tanganyika "territory" wanakwambia umemsikiliza Profesa Anna Tibaijuka, nenda kasome mwenyewe.

Hayo ndio majibu ya chawa, kwa hiyo Mimi mwenye digrii mbili naulizia bila kusoma!? Labda angeniambia mimi sio mbobevu wa sheria ningemuelewa, lakini bila ubobevu wa sheria nikisoma mwenyewe nagundua mkataba unatufunga kuanzia kwenye article 4 scope of co-operation,areas of co- operation, description za phase 1 na 2.

-Phase 2 inazungumzia "territory" Anga,bahari na nchi kavu.

Phase 1 projects, development, Management and operation of Dar es Salaam port, kusimamia shughuli na kuendeleza bandari ya Dar es Salaam, Phase 2 of projects inataja maeneo (development of logistics platforms, special economic zones, industrial parks and other logistics infrastructure to support trade and transit corridors servicing land locked countries in East Africa and southern Africa) hapa ndipo tunasema Mkataba unahusu "territory" yaani mkataba utaanzia kwenye mipaka ya Tanzania Nungwi, Pemba na unguja, mkataba utakuwa juu ya territory ya Tanzania anga, bahari na nchi kavu, mkataba unasema Tanzania itaijulisha Dubai juu ya fursa zozote zilizopo, na zitakazokuwepo, hili ni sawa na kusema Watanzania hatuwezi chochote,sasa chawa wanasema bandari ya Dar es Salaam peke yake sijui wao kama wamesoma mkataba, tafadhali chawa msiseme watu hawajasona mkataba kumbe ninyi ndio hamjasoma mkataba, chawa sawa na kupe mnafikia kumjibu hata Profesa Shivji,hii ni ajabu sana, sijui Tanzania yetu inakwenda wapi!?

-Nukuu za Profesa Shivji.

"Mkataba huu hauwezi kuvunjwa kwa sababu zozote zile hata kama tumevunja uhusiano wa kidplomasia na U.A.E (Falme za Kiarabu)" Prof. Issa Shivji

"Imezungumzwa sana kwamba watu wetu wataendelea na ajira zao, wafanyakazi Watanzania watashiriki vipi katika management (usimamizi)?, wafanyakazi wa kawaida (makuli) na HR (Afisa Rasilimali Watu) hawa watakuwa Watanzania lakini wengine wote katika management watatoka Dubai (DP World)" Prof. Issa Shivji

"Mikataba ya miradi (project agreement) na nchi mwenyeji (host government) mikataba hii haitapelekwa bungeni wala haitawekwa hadharani kwa sababu ni siri. Mkataba huu (wa uendelezaji wa bandari ) ulipelekwa bungeni kwasababu ni mkataba wa kimataifa lakini project agreement ni ya kibiashara hivyo ni confidential (siri). Watanzania hawatajua wameingia katika mkataba gani na kuna nini ndani ya mkataba na mkataba umesema nini" Prof. Issa Shivji

"Shughuli zilizotajwa katika awamu ya kwanza (ya mkataba wa bandari) sio za bandari pekee, kuna Special Economic Zone (maeneo mahususi ya kiuchumi), trade corridor, free zone" Prof. Issa Shivji

"Eneo ambalo sio la DP WORLD lakini ni karibu na eneo la DP WORLD, mtu akitaka kujenga barabara au flyover ambayo interfere (itaingilia) shughuli za DP WORLD hairuhusiwi kwa mujibu wa mkataba huu (wa uendelezaji wa bandari). Serikali itahakikisha kwamba shughuli hizo hazitokuwepo kando kando na eneo la DP WORLD" Prof. Issa Shivji

"Kwa mfano serikali ina dhamira au haina dhamira ya kudevelop (kuendeleza) bandari ya Tanga au Mwanza kwa mujibu wa mkataba , DP WORLD wana haki ya kupewa taarifa hizo kabla ya yote ili wakitaka waweze ku-express interest (kuonesha nia)" Prof. Issa Shivji

"Kuna sekta nyeti katika uchumi na huwezi kuweka katika makampuni ya watu binafsi na bandari ni sekta nyeti mojawapo, ni roho na mishipa ya uchumi hivyo huwezi kuweka katika mikono ya watu binafsi kwa sababu mbalimbali" Prof. Issa Shivji

"Mali zetu ikiwemo madini tunazo-export (tunazozisafirisha nje) ma mali tunazozileta zinapitia bandari na mali nyingine ni very sensitive (nyeti sana), huwezi kuweka hiyo mikono mwa kampuni mbinafsi bila wewe kuwa na mamlaka" Prof. Issa Shivji

Nikiishia hapa, Mimi ni
Msemakweli Chakubanga,
Dar es salaam.
0755078854

-Bachelor of business administration in International business.

-Master of Leadership and Management

Recent Publications;-
Assessment on the Effects of Micro-financing on Poverty Reduction.
 
Hizo nukuu ni Kwa ajili ya Dpworld Tu?
Wakati wa Ticts kulikuwa hakuna hizo risks???
Au Dpworld ndo "analeta hatari"??
 
Kitu cha kukiangalia hivi sasa ni kundi la wasomi,wabobezi na manguli wa sheria kupinga mkataba huu,halafu kuna mtu anaamka alipokuwa amelewa ofa za mwarabu anasema wasomi na wabobezi hao hawajasoma mkataba,haya ni maneno yaliyotumika enzi zile waliokuwa wanapinga mkataba ni wavuja jasho,walalahoi,washinda njaa,makabwela na watwana, tofauti ya upingaji wa leo,wapingaji na Vyuo vikuu,wasomi, Maprofesa, Madaktari wa falsafa,manguli na wabobezi wa sheria,kundi hili kwa namna yoyote sio la kudharauliwa hata kidogo.
 
Hizo nukuu ni Kwa ajili ya Dpworld Tu?
Wakati wa Ticts kulikuwa hakuna hizo risks???
Au Dpworld ndo "analeta hatari"??
Kipengere no.7
Kuna utofauti wa TICTS na DP-WORLD na wakati TICTS inapewa kazi hakukua na mjadala sababu sheria za wakati ule zilikua tofauti na ilivyosasa.Kulikua na mabadiliko ya sheria 2017 wakati wa sakata la makinikia yaliyozaa hoja zile kuwa nchi itashtakiwa nk zilizotolewa na kina lissu bungeni wakati ule.
 
Hizo nukuu ni Kwa ajili ya Dpworld Tu?
Wakati wa Ticts kulikuwa hakuna hizo risks???
Au Dpworld ndo "analeta hatari"??
Kelele kwa watawala hazikuanza leo kwenye issue za uwekezaji pale kunapokua na sintofahamu kwa umma.Hizo Kelele zilisikika toka suala la Loliondo(loliondo gate) Bulyakhulu,Richmond, IPTL,Escrow, EPA nk nk.Nimekukumbusha hapo kuwa 2017 tulibadili sheria ili kuondoa baadhi ya vipengere vilivyokua na udhaifu vilivyopelekea nchi kuingia kwenye mikataba ya hovyohovyo isiyozingatia maslahi ya umma.
 
Hizo nukuu ni Kwa ajili ya Dpworld Tu?
Wakati wa Ticts kulikuwa hakuna hizo risks???
Au Dpworld ndo "analeta hatari"??
Kwenye TICTS uliona mkataba wake ukiwa kama huu wa kuuza nchi?

TiCTS alikuwa port operator na hata DP World angekuja kwa Terms of reference kama za TICTS, wala Watanzania hasa Watanganyika wala wasingegombana nae.

Mkataba huu wa DPW, unaingilia sovereignty yetu. Period
 
Back
Top Bottom