Elius W Ndabila
JF-Expert Member
- Jul 17, 2019
- 324
- 649
Kwanza utaona ujinga wa baadhi yetu juu ya kupambanua mambo makubwa ya Taifa. Nimetumia ujinga kwa kuwa "UJINGA" siyo tusi bali ni ukosefu wa maarifa ya kitu fulani ambacho hukijui. Ukishafundishwa ujinga unapotea.
Pili nimeona upande wa pili ambao ninaweza kusema hoja zao ukizipima zinajengwa sana kwenye aya yangu ya kwanza ya "UJINGA". Ila kila binadamu ana ujinga kwenye mambo fulani fulani, hakuna binadamu anayejua kila kitu. Leo ninazungumza ujinga unaotokana na uchambuzi wa ripoti ya CAG. Kuna watu nimeona wakiandika kuwa CAG amelenga kumchafua Hayati JPM. Yaani wanaona CAG anawaonea wakwapuji wa mali za umma kwa kuwa lengo ni kumchafua JPM.
Hakuna mtu mzuri asilimia Mia. Kila uzuri una upande wa ubaya. Mimi ukiniuliza nitasema JPM alikuwa Rais bora Afrika. Makosa yote aliyoyafanya alifanya kwa wivu wa kutaka Tanzania kuwa donor country. Lakini pamoja na haya, bado haiondoi dhamira ya CAG Kuibua madudu mengi yaliyofanywa na wasaidizi wa JPM. CAG hana nia ya kumchafua mtu, bali kutimiza takwa lake la kikatiba Ibara ya 143(3).
Tusome ripoti, tuichambue na vyombo vingine Kama TAKUKURU wachunguze juu ya hoja hizo. Mapenzi yetu kwa hayati yasiondoe nia njema ya CAG kutaka kulisaidia Taifa zaidi. Ni "MJINGA" tu anayedhani CAG anamuonea mtu. Tusubirie uchunguzi ndipo tutajua nani kaonewa na nani hajaonewa. Hizi fedha ni zetu lazima tujue ukweli wake.
Juu ya miradi Kama SGR, Standard Geurge n.k hata Kama tulikosea mimi ninashauri iendelee kumaliziwa kwa kuwa mpaka sasa tumeshatumia fedha nyingi. Kubwa tu mfumo wa kuijenga ibadilishwe na kuhusisha taasisi kubwa duniani ili mifuko yetu isiendelee kuwa empty.