Habari nitaelezea kwa experience yangu
Nilipoteza cheti cha kuzaliwa na cha form 4 mwaka 2014
Cheti cha kuzaliwa ilikua rahisi tu nenda office za ustawi wa jamii zilizopo karibu nawe au za RITA waambie watakutengenezea kingine
Kimbembe kipo kwenye cheti cha form 4 niliteseka sana. Kwanza make sure una loss report ya polisi, then weka tangazo la upotevu wa cheti chako kwenye gazeti.
Then chukua hio loss report na tangazo la gazeti nenda office za NECTA dar es salaam, utalipia kama skosei 100k
Utapewa cheti kingine cha form 4 ila pale juu kinaandkkwa “DUPLICATE” wakimaanisha kuwa umepewa copy ya pili. Ondoa shaka cheti hicho kinakubalika kiko sawa tu na kile cha kwanza kasoro maneno “DUPLICATE” pale juu
Changamoto ipo kwny kukipata sasa, nilifuatilia zaidi ya miaka 2 napigwa kalenda mpaka nkakata tamaa. But nikaja kupewa now niem relax
Nashauri ingia website ya NECTA utaona utaratibu wa kupata vyeti kwa wale waliopoteza