Ukiritimba umekithiri Hospitali ya Wilaya Misungwi

Ukiritimba umekithiri Hospitali ya Wilaya Misungwi

Duduvwili

JF-Expert Member
Joined
Jan 31, 2015
Posts
4,355
Reaction score
4,476
Wakuu Umuofia,

Kama heading inavyojieleza hapo juu napenda kuwasilisha malalamiko yangu kwa yeyote anaehusika nimewasili katika hospitali hii ya wilaya kwa minajili ya kumtibia mke wangu lakini cha ajabu ni kwamba ni zaidi ya saa mbili sasa hakuna huduma yoyote niliyopatiwa zaidi ya kukabidhiwa kadi ya tembo afya lakini hakuna kinachoendelea kwa kile wanachodai ni hakuna mtandao hivyo kusababisha foleni.

Ombi langu ni kwamba kwanini kusiwe na mbadala wa hicho kinachoitwa mtandao?

Ikumbukwe wengine wanakuja hapa wapo sirias kimyakimya mfano hawa wanawake unakuta mtu anamaliza pedi2 bila kupata huduma na yupo hospitali

Naomba mlitizame kwa jicho la tatu suala hili
 
Kituo cha afya hicho haina hadhi ya kuwa hospital ya wilaya...halafu kituo kimejaa medical attendant wa darasa la saba na hao ndio majipu wanaosababisha kituo kionekane kama shamba la bibi....na wanarogana balaa...

Yupo jamaa yangu ni afisa tabibu wa siku nyingi hapo lakini ninavyoandika hapa jamaa anaumwa ni mwaka sasa yupo kitandani na ugonjwa haueleweki..
 
Kituo cha afya hicho haina hadhi ya kuwa hospital ya wilaya...halafu kituo kimejaa medical attendant wa darasa la saba na hao ndio majipu wanaosababisha kituo kionekane kama shamba la bibi....na wanarogana balaa...yupo jamaa yangu ni afisa tabibu wa siku nyingi hapo lakini ninavyoandika hapa jamaa anaumwa ni mwaka sasa yupo kitandani na ugonjwa haueleweki..
Mkuu kuna shida gani hizi wilaya za kanda ya ziwa?hususan Kwimba nako Afya kipengele yamewahi kunikumba pia pale Ngudu hospital napo ni majanga tu
 
Back
Top Bottom